Mimi nashauri UKAWA kufikiria kumpitisha Profesa Ibrahim Lipumba kugombea urais kupitia umoja huo kwani anafaa na ananguvu. Kwa upande wa CHADEMA itakuwa ni heshima kubwa kama watakubali kumuachia Lipumba kuchukua nafasi hiyo na hivyo kuondoa dhana kuwa wao wanataka kudominate ndani ya UKAWA kwani ni wazi upande wa nafasi za ubunge na udiwani wao watakuwa na nafasi nyingi kutokana na umaarufu wao hasa upande wa Tanganyika. Ikiwa Lipumba atapitishwa UKAWA itakuwa na uhakika wa kura nyingi kutoka Zanzibar na Tanganyika.