Mike T alikuwaga funiko bovu na lafudhi yake
Kweli kweli mkuu ukimchukua ile flow yake ya tulikulaga,tulikwendaga basi tu ...bila kumsahau kichwa cha ubunifu mzee wa mabinti wa magetini na k'nyama a.k.a J.Mo utapenda
We miss you all.
Juzi nimesikia wimbo wa mkoloni na Dk. John dah.. usipokuwa makini utadhani wanatukana, utata mtupu mara kunyonyana, kusimamisha, kutia mkazo yaani duh..!
kuhusu wimbo wa jwtz ule wimbo sio wa jay moo ule wimbo unamilikiwa na jeshi lakini aliyepewa dili aimbe ni nature yeye akaona ni busara awashirikishe jay moo na prof jaymtoa mada naona hufatilii game ya bongo wewe..... wagosi wa kaya wamerudi tena na wimbo unaitwa bao... jay moe karudi na wimbo unaitwa JWTZ kamshirikisha prof jay na juma nature utafute youtube kuna kipande cha video hiyo..... nature pia na wimbo kama jana...... prof jay ft diamond wimbo kipi sijasikia..... mwana fa sio msanii huyo....d knob pia karudi na kazi inaitwa nishike mkono ft mwasiti na ukitaja marapa wafu wa kwanza jaffarai
kuhusu wimbo wa jwtz ule wimbo sio wa jay moo ule wimbo unamilikiwa na jeshi lakini aliyepewa dili aimbe ni nature yeye akaona ni busara awashirikishe jay moo na prof jay
Wakongwe njooni mrudi mkaikomboe fani,mmeondoka mkaliacha gemu mikononi mwa hawa madogo sahivi muziki wa bongo umepoteza taswira yake na mliowaachia wamefika sehemu hawaelewi hata wao wanakwenda wapi
Rai yangu ni moja,rudini kwenye gemu muiweke sawa fani hii
cc:Mezz B,Mkoloni,D.Nob,Nura,Mwana FA,Jaffarey ..njooni jamani jahazi limekosa wakongwe! njooni mtoe darasa kwani bado ngoma zenu zinabamba mbaya sana.
93.7 FM itarudisha game ya kale na kuwathamini wasanii wa kale