Ab-Titchaz,Smatta,Masanja,...
..jamaa aliyekuwa appointed kuwa mkuu wa polisi alikuwa mkuu wa GSU kabla ya hapo.
..kwa uelewa wangu GSU ni sawasawa na FFU kwa upande wa Tanzania.
..sasa najiuliza, hawa GSU hawakutesa wananchi kwenye zile vurugu za uchaguzi?
..nauliza hivyo kwasababu huku kwetu Bongo si rahisi kukatokea maandamano kama yaliyotokea Kenya na FFU wasishiriki kuyashughulikia/kuyazima.
Joka Kuu,
Heshima mbele.
Hawa GSU ni kama FFU na zaidi sanaaa!!! Hawa jamaa wako fully
masinondo...more like a small army of sorts. Mostly they do the President's
dirty work na walitumika katika zile fujo za uchaguzi wa '07 kuleta 'adhabu'
katika maeneo ambayo Kibaki alikua anaona wanaleta 'utundu'. Wakati wa
enzi zetu chuo kikuu Nairobi, Rais Moi alikua anapenda kuwaleta maeneo
anytime we made 'noise'. Wanafunzi wengi waliuwawa katika mikono ya
hawa mabwana na kesi zao zilipotelea mahakamani wakati ule hadi leo.
Kwa taarifa yako na wengineo, hii appointment has nothing to do with
competency of the individual bali Kibaki is manouvering in the background
kuleta distractions. Kwa sasa issue kubwa Kenya ni ile ya majina ya watu
kupelekwa The Hague, thanks to Jaji Waki na Koffi Annan. Kwa vile jamaa
walikua wamechelewa kuunda local tribunals to try the suspects of the
violence of '07, mpira ukasogezwa mbele. Baadaye Kibaki na Raila
wakamuomba Prosecutor Ocampo m'da zaidi wa kuunda hio tume na kupitia
ushirikiano wa wabunge. Wabunge kwa idadi kubwa wakachomoa na
seketa ikarudi palepale. Kwa ufupi, nataka nikupe ahadi ya one hundred
percent kua Ocampo will proceed with whatever he has to do because
Kenya right now cannot decide which way to go with this situation.
Ishu ya pili ni kua juzi huyu Rais Kibaki alimteua Justice Aaron Ringera
kuendelea kuongoza Kenya Anti Corruption Commission (KACC) ambayo
kwa ufupi iliundwa kwa makusudio ya kupiga vita ufisadi. Lakini acha
nikuhabarishe na usicheke....up to today hawa jamaa hawajafanya lolote
la maana in there fight against corruption na wanaingiza mshahara wa karibu
milioni 5 za Kenya kwa mwezi!!!!....badili kwa hela ya madafu mkuu. The
appointment of this guy inasemekana inatakiwa kua kupitia recommendations
za bodi flani. Kisha kunakua na vetting process ya kiaina kabla hajapewa kazi.
Kumbuka pia tunaambiwa kua serikali ya Kenya ni ya Muungano baina ya
Raila/ODM na Kibaki/PNU lakini la kuchekesha ni kua Raila na ODM kwa jumla
was not consulted on this matter (as well other critical appointments) which
is of such national importance.
Bunge limegoma na hii appointement ya huyu bwana Ringera na unaeza
kusoma zaidi hapa
HOUSE TEAM SAYS KIBAKI ACTION ILLEGAL.
ama
ANOTHER MOVE TO STOP RINGERA AS MP FILES SUIT.
kwa hivyo against this background Kibaki atoa hii kali ya kumtoa jamaa
kama mkulu wa Polisi na kumpeleka shirika la posta. Maybe he wants it to
serve as distraction lakini kumekucha Kenya!
The next few weeks will interesting to watch the goings on across the border.
Shukran.