Ndugu zangu mimi ni kijana mwenye miaka 31. Ni zaidi ya miaka mi5 sasa nimekuwa na maumivu katikati ya maungio ya kiuono na mbavu.
Dalili nilizo kuwa nasikia
1. Uchovu wa mara kwa mara.
2. Kujisaidia haja ya mviringo kama mavi ya mbuzi.
3.Maumivu ya kiuno.
4. Kupata choo kigumu hivyo kusababisha kutumia nguvu kusuma haja.
5. Kuna joto fulani kama la kiungulia hivi haliumi sana ila linakera.
6. Kuna muda nikila sana chakula cha wanga sana, chumvi ama pili pili joto hili huongezeka.
Nilifanikiwa kwenda hospital nilifanyiwa kipimo kinaitwa choronoscopy na kugundulika kuwa nina uvumbe kwenye utumbo mpana, kwa maelezo yao ni uvimbe mdogo sana. Hivyo nina takiwa kubadilisha aina ya vyakula tuu yaani nile mboga mboga za majani kwa wingi.
Sikupewa dawa. Zaidi ya mwongozo huo.
Nimewasiliana na watu wa tiba za asili. Wengi wao wameniambia kuwa hii ni bawasili ya ndani na watanipatia dawa na kupona kabisaa.
Kabla sijafika mbali. Kuna mtu yeyote alishawahi ama anaumwa kama hivi? Je experience ni kama hii ama kuna utofauti?
Kuna mtu ambae aliumwa na kupona kabisa huu ugonjwa?
Asanteni!