Umenena vyema mkuu kifutwe kipo kudhurumu watu kimeacha mauzui ya uanzishwaji wake kimekuwa Cha mavuno kwenye lami hata Kama mazao hayastawi kwenye lami wao ni kuvuna tu wabaya hawa wanyang'anyi kabisa harafu wanavyonuna ukiingia 18 yake utapenda
Nani atakifuta hicho kitengo wakati kwa sasa wanashindani kukusanya mapato. Na kipimo cha mkoa bora ni makusanyo mengi kama dalili ya kushughulikia madereva?
Nafikiri Matrafiki ni binadamu lakini inaonekana kuna Presha kubwa nyuma yao ya kukusanya pesa kila siku na wanatumia mwanya huo huo kuwa miungu watu.
Lakini pia Sheria ni tatizo mana kila kosa limekua linaadhibiwa kwa faini. Na makosa madogo madogo ni Mengi na yote ni faini tu kulingana na sheria. Sasa hawawezi kukosa kosa hata kama ni dogo na halina madhara kwa usalama.
Mfano Mtu anaandikiwa faini kuwa hajasimama kwenye Zebra Crossing hata kama hakuna mtembea kwa miguu. Huu mwanya wa kisheria na hakuna Kiongozi anayeuona kwa sababu wao wanamaisha mazuri na hawakamatwa hivyo hayo hayawahusu.
Jambo lingine ni suala la Mwendo kasi wa 50 kwenye makazi hata kama barabara imenyooka nayo sio sawa. Wanapaswa sasa kuongeza ifike 70 KPH kama hakuna kibao lakini kuna makazi lakini pia Makazi yanatofautiana hivyo vibao visiwewe 50 tu. Sehemu nyingine viwe 60 ,70.
Mabasi yaongezewe speed ifikie 90 KPH na 100 sehemu iliyonyooka. Vibao ndio viongoze madereva barabarani sio sheria kwenye vitabu tuu.
Pia pawe na mahakama maalumu ya makosa ya barabarani ili watu wasionewe.
Watu wajiamini ili askari anayembambikia MTU Kesi au kumwonea akishindwa mahakamani alipe fidia kwa mwananchi ili kuongeza uadilifu.
Mara nyingi naona nchi nyingi za kiafrika zina matatizo hasa kwa wananchi wa Chini kwa sababu viongozi wao ni mabepari ,wakoloni na miungo wasioishi kwenye dunia Moja na wananchi wao pamoja na kujigamba kuwa wanawajali wanyonge.
Labda siku moja atokee ,mkuu wa nchi ,Waziri mkuu ,mawaziri, spika wa Bunge na wabunge Watoke Dar es salaam mpaka Dodoma kwa kutumia barabara halafu wafuate alama za barabarani za kudhibiti mwendo . Kwenye speed 50 watembee 50. Hakika wangeborka sana na wangebadili mawazo na kufanya utafiti upya wa namna ya kubadili baadhi ya sheria za barabarani .
Vinginevyo tutabaki kuwalaumu Trafiki ambao ni vijana wanyonge tu wasio na maamuzi ya kubadili sheria zaidi ya kusimamia sheria mbovu zilizopo ili kulinda kibarua chao.