Polisi wakusudia kumkamata John heche wasema wanataka Kumuhoji

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amekiambia kituo cha Habari cha EATV kuwa, afya ya mbunge wa Bunda Mjini Ester Amos Bulaya, kuwa hali yake si nzuri akiwa mahabusu kwani presha yake imeshuka, na kwamba hajatoka tangu alivyopelekwa jana.

Jana Ester Bulaya alikamatwa na polisi kwa kosa la kuhudhuria mkutano wa mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, na mpaka sasa hajaachiliwa, huku mwenzake John Heche akitafutwa na polisi.

Wakati huo huo, Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mh. John Wegesa Heche, anatafutwa na jeshi la polisi mkoani humo, kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi mpaka sasa.

Tumaini Makene, amesema John Heche ametakiwa kufika polisi leo hii jioni.
 
Reactions: BAK
Hiyo ndiyo Sera ya viwanda, haya ngoja tusubiri hivyo viwanda
 
Aende tu anaogopa nn? C wana mwanasheria msomi atatetewa tu atatoka.
 
Kosa lake ni KUHUDHURIA MKUTANO?
No wonder!
Kwa akili hii, hata Lugumi akitushtaki tutashindwa tu maana vipaumbele vyetu ni vya hovyo hovyo.
 
Reactions: BAK
Nchi ya ajabu sana hii. Kupanda jukwaani kwenye "eneo lisilo lako" sasa ni kosa la kumlaza rumande siku 2 Mbunge wa JMT? Kapuku kama mimi hali itakuwaje sasa? Mbona lile zeze Polepole linapanda popote tu? We are slowly heading towards apartheid era
 
Polisi Kanda Maalum Tarime-Rorya wakiwa kwenye magari 4 na silaha wamezunguka mkutano wa hadhara wa CHADEMA, Sirari,Tarime Vijijini muda huu

Hadi sasa Jeshi la Polisi Tarime-Rorya hawajasema wanamtafuta Mbunge Mhe. John Heche kwa ajili ya kitu gani hasa
 
Kichwa cha habari tofauti na habari iliyopo ndani.Hata wewe Mwanahabari?
 
Wameahidiwa vyeo kama yule formal RPC wa Dar

Psalm 133:1
"Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…