Danisamweswa
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 453
- 154
Jeshi la Police linalopokea amri kutoka hata kwa Katibu wa CCM wa Wilaya / Mkoa ni hatari sana kwa usalama wa nchi.
maneno yako uliyoyasema ni sawa kabisa mwanangu lakini polisi wa nchi hii hawako kwa ajili ya kulinda wananchi kama ufikiriavyo wewe,polisi wa nchi hii wako kwa ajili ya kulinda maslahi ya ccm tu, kinana anaadamana na watu chungu mzima katika ziara zake na anapokewa na watu kibao lakini huta sikia hata siku moja wanakatazwa na polisi,sisi kina gogo la shamba tulikwisha sema siku nyingi kwamba watakaoleta vurungu katika nchi hii ni polisi na wala sio wananchi na yote hayo yanatokana na utawala wa ccm na serikali yake,jicho lingine wanaloangalia ccm wanategemea polisi wakishindwa watatumia jeshi la wananchiNi jambo linalosikitisha kuona kuwa Jeshi letu la Polisi badala ya kuwa chombo cha kulinda raia na mali zao kinageuka kuwa chombo cha kuumiza raia na kuharibu mali zao. Jambo hili nimeliona wala siyo mara moja. Tukio la jana makao makuu ya polisi jijini Dar lilikua tukio la hovyo na la aibu kwa nchi yetu. Watu wamemsindikiza mwenyekiti wao wa Chama Chao wamekaa chini kwa amani kabisa polisi wanawafukuza na mbwa kama vile wamekuwa swala. Hili jeshi linalinda amani kwa mtindo huo au linavuruga amani?
Ni kigezo gani kilichotumia wa polisi kuwafukuza wanachama wa CHADEMA na hata kuwapiga waandishi wa habari? Ninapata shida kuwa jeshi hili linashindwaje kufanya kazi zake kwa weledi? wangekuwa ni wanachama wa CCM wamemsindikiza mwenyekiti wao jeshi la polisi lingefanya walichokifanya jana?
Kwa nini jeshi la polisi lisijitenge na siasa? Polisi wanalinda nani? Wananchi wanapokasirishwa na kinachoendelea dodoma wanataka kufanya maandamano polisi wanasema maandamano hayo ni haramu? Nani asiyoeona uharibifu wa fedha unaoendelea dodoma kwa kisingizio cha bunge la katiba? Siyo halali wananchi kuonyesha kutokuridhika kwao kwa maandamano?
Nguvu inayotumika kuzima maandamano ya amani kwa nini zisitumike kuzima uahalifu katika nchi hii na kupambana na majangili wanaomaliza tembo zetu? Iko haja kwa jeshi la polisi kujitoa kwenye ushabiki wa vyama vya siasa. Lisipofanya hivyo litahatarisha usalama na amani ya nchi yetu. Badala ya kuwa walinzi wa amani litageuka kuwa wavurugaji wa amani. Picha ya namna hii haifai kwa jeshi letu la polisi.
Ni jambo linalosikitisha kuona kuwa Jeshi letu la Polisi badala ya kuwa chombo cha kulinda raia na mali zao kinageuka kuwa chombo cha kuumiza raia na kuharibu mali zao. Jambo hili nimeliona wala siyo mara moja. Tukio la jana makao makuu ya polisi jijini Dar lilikua tukio la hovyo na la aibu kwa nchi yetu. Watu wamemsindikiza mwenyekiti wao wa Chama Chao wamekaa chini kwa amani kabisa polisi wanawafukuza na mbwa kama vile wamekuwa swala. Hili jeshi linalinda amani kwa mtindo huo au linavuruga amani?
Ni kigezo gani kilichotumia wa polisi kuwafukuza wanachama wa CHADEMA na hata kuwapiga waandishi wa habari? Ninapata shida kuwa jeshi hili linashindwaje kufanya kazi zake kwa weledi? wangekuwa ni wanachama wa CCM wamemsindikiza mwenyekiti wao jeshi la polisi lingefanya walichokifanya jana?
Kwa nini jeshi la polisi lisijitenge na siasa? Polisi wanalinda nani? Wananchi wanapokasirishwa na kinachoendelea dodoma wanataka kufanya maandamano polisi wanasema maandamano hayo ni haramu? Nani asiyoeona uharibifu wa fedha unaoendelea dodoma kwa kisingizio cha bunge la katiba? Siyo halali wananchi kuonyesha kutokuridhika kwao kwa maandamano?
Nguvu inayotumika kuzima maandamano ya amani kwa nini zisitumike kuzima uahalifu katika nchi hii na kupambana na majangili wanaomaliza tembo zetu? Iko haja kwa jeshi la polisi kujitoa kwenye ushabiki wa vyama vya siasa. Lisipofanya hivyo litahatarisha usalama na amani ya nchi yetu. Badala ya kuwa walinzi wa amani litageuka kuwa wavurugaji wa amani. Picha ya namna hii haifai kwa jeshi letu la polisi.
Maneno kama haya ya kipuuzi kaongee na mke wako, halafu nchi haijengwi na watu wa aina yako, wangapi wamekufa enzi za ukoloni na kutafuta uhuru kuifanya tanzania hapa ilipo na hawakutawala leo umekalia mkia unajiona mpenda amani kumbe una maslahi yako binafsi.Huyo mwandishi hakuwa na jacket la kumtambulisha, haya, kaitwa mbowe, nyie wengine mnakwenda kujazana bila sababu, mnaambiwa tawanyikeni hamtaki, hv nyie au ndugu zenu wakiitajika polic mbowe huwa anawasindikiza??
Huyo mwandishi hakuwa na jacket la kumtambulisha, haya, kaitwa mbowe, nyie wengine mnakwenda kujazana bila sababu, mnaambiwa tawanyikeni hamtaki, hv nyie au ndugu zenu wakiitajika polic mbowe huwa anawasindikiza??