jaffari odhiambo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 526
- 13
Polisi na maliasili Bunda wamechachamaa kukamata wanaoleta mkaa mjini hapa jana na leo. Polisi na hao maliasili wanawasaka waleta mkaa kwa kutumia gari la maliasili na wakiwakamata wanachukua na baisikeli zao.
Jamani hili suala linakera sana maana hao wanaoleta mkaa sio wakataji wa moto maana wao wamenunua ili wauze na kupata angalau pesa ya matumizi. Sasa kama hali ya kijijini ni ngumu vile tujuavyo kweli hawa sio kwamba wananyanyaswa?
Halafu huo mkaa wanagawana na ukibaki wanauza na kugawana pesa. Je, mbona wao sasa wanauza?
Wacha uzushi we mtoto ws kiume.
Biashara ya mazao ya misitu tanzania nzima imeingia mkenge, ---- mawakala wa misitu wanaitwa TFS, kazi yao ni kuhakikisha misitu haiharibiwi ambapo madhara yake kila mtu anayajua. Kuepuka kamatakamata hyo ni kuwa na lessen ya uvunaji ili uvune kihalali.
Si kweli kuwa wanagawana pesa hizo, labda kama umefanikiwa kuwashawishi rushwa, wakiuza wanauza kwa bei ya serikali na hivyo kuongeza makusanyo.
Mlisha kalili kuwa polisi waonevu basi tu mmawapinga hata kwa suala jema
Kama kijijini kuna maisha magumu serikali iruhusu uchomaji wa mkaa na kumaliza misitu?.eti wawakamate wachomaji hivi unajua uchomaji mkaa ulivyo? Mimi nimewahi choma mkaa kabla ya kuwa kolokoloni kiukweli kutukamata ni ngumu mno kwani huwa tunaweka watoa taarifa kila kona kuwa wakiaona askari wanakuja msituni watujulishe na kweli tulikuwa tulikuwa tunajulishwa na hatukamatwi ila walipoanza kukamata wabebaji mkaa tu mambo yakawa magumu sana maana mkaa ukakosa hivyo niliacha hiyo kazi kuepuka jela
Wewe usiseme watu wamekariri yawezekana ana uhakika na anachokisema.
Mkuu miondombinu iliyopo ni ya mkaa kuchomwa tu! umewahi kujiuliza ni watanzania wangapi wanaotumia mkaa kupikia? Hivi ikitokea mkaa ukapotea ghafla mjini hali za watu zitakuaje. Zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanaoishi mjini wanategemea mkaa kupikia, huwezi kuokoa misitu bila kua na nishati mbadala ya uhakika.
Tatizo ni uamuzi wanani awe kiongozi pale bunda. Walishindwa kuchagua mbunge sahihi sasa acha wakome ubishi.
Tena nasikia ndiyo wilaya ya mwisho kwa umasikini Tanzania.
Mlipokea kanga na chumvi na vibukubuku ndo sasa vinawatokea mapuani.
Hakuna cha bure zaidi ya maisha bora kwa kila mtanzania kupitia T 2005-2015 Kikwete tumechoka, pinda liwalo na liwe-a.k.a wapigwe tu.