Polisi achoma guard post

OMEGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
693
Reaction score
301
Nilikuwa safarini Sumbawanga na Mpanda,nilipofika Mpanda nikahamua kwenda CRDB kuchukua vijisenti kabla ya kuendelea na safari Tabora.CRDB Tawi la Mpanda ni kati ya Majengo mapya ya kisasa kabisa,nilishangaa kukuta Kibanda cha walinzi hapo gaitini kikiwa kimeungua moto,ni kibanda kipya kabisa kilichojengwa kisasa lakini tayari kimeungua moto,nilipouliza wadau wakaniambia kuwa polisi mmoja mvuta bhangi alidondosha kipisi kwenye godoro kisha yeye na mwenzake wakatoka nje ya lindo kwenda kutafuta wanawake kurudi walikuta Kibanda kinateketea,kwa kweli inasikitisha sana,inabidi polisi wachukue hatua za maksudi kuthibiti ongezeko la polisi wapya ambao asilimia kubwa ni wavuta bhangi,inatia aibu unapokutana na polisi in uniform amekaa kijiweni anapuliza ya Arusha,ikibidi katika vipimo kabla ya kwenda CCP wongeze kipimo cha damu kama mtu ni mtumiaji wa banghi au drugs,vinginevyo tunakoelekea ni kubaya sana.Naomba kuwasilisha wakuu
 
Tatizo our country is rotten at heart!, kuna mshkaji i happened to attend the same class with him na alikuwa anapiga sigara kubwa kwa saana, nilishangaa kumuona u/wa taifa kwny sherehe
 
Naona ajabu unashangaa kuwa mapolisi wanavuta bangi Tanzania!! Nchi hii imeoza kiasi kwamba ina mawaziri wavuta bangi na wengine mawaziri maharamia wanatembea na silaha za kivita lakini kiongozi wao haoni wala hasikii kuwa hayo ni maadili potofu kwa viongozi serikalini!!!
 
Maadili hakuna kuanzia chuo cha Polisi wanapofundishiwa ndiyo kumeoza kwasababu kama maadili yapo asingeweza kufika mkoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…