Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,900
- Thread starter
-
- #21
sababu ya tanganyika kuendelea na muungano wa zanzibar ndo kama hii kudumisha mila na desturi za kibantu na kuondokana na ule ukiritimba wa kimanga wanaofanyiwa wabantu wenzetu huko visiwani
Kuna mirija mitatu ya kufyonza pombe pale, moja ya Pinda, moja ya yule mama na nyingine ya Makamu wa Rais, usipindishe habari, kwani kesho tukikukuta upo unavinjari eneo la machangudoa maana yake unafanyia mahesabu ya kuwapata.
Na huo mtungi kuna siri ile ya maana ya kusumbawanga na maana yake ukitaka kujua nenda pale Mazwi watakueleza maana ya wanga, kule mji mwema mchanganyiko hawajui maana ya sumbuwanga. Ukidharau na kuendelea na safari baada ya kuvuka gati la wanyamapori la Katavi gari likigoma kupanda mlima wa Lyamba lya Mfipa usijejutia.
Kuhalalisha hilo ipo siku ataenda kukagua mashamba na kukuta bangi ikitumiwa na wakinga kama kiungo cha mboga za majani na kushiriki itakuwa ni busara zaidi? Maana cheo si kinga ya uvunjaji wa taratibu za mila, afya na kanuni.
Hiyo haina kufundisha.Anaijua vizuri.usiku wake alimfundisha kula kiti fire
Nimepita pale getini Katavi juzi nikiwa peke yangu na drive hakuna kilichotokea, na sasa hivi nipo Mlowo.
Kuhusu Nguruwe na Bangi, hapo nadhani unajichanganya kama si kuchanganya mambo. Bangi ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi na mtu hatakiwi kuitumia by any means, wakati Nguruwe ni haramu kwa mujibu wa sheria za kiimani na unaruhusiwa kula kidogo kama una njaa.
hata bia ni maji taka
Kumbe ndo mana macho ya Pinda yako vile yalivyo, Chimpumu si mchezo nduguzanguni
Kuna jambo moja muhimu hapa kuelewa juu ya nafasi na mzingira ambayo kiongozi mkubwa kitaifa anatakiwa awe mfano si wa kutunza utamaduni tu ila kutoendekeza mambo ambayo hurudisha nyuma maendeleo.
Kesho hao hao watashinda vilabuni kwa hoja kwamba mbona Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu wakifika tunawaadalia pombe na wanakunywa, iweje sisi? Busara ni jambo muhimu sana..
Nimeongea mara kadhaa kuwa mwana CCM maana yake umechagua kupoteza mwelekeo sahihi wa kufikiri, na hatima yake ndio haya tunayoshuhudia sasa. Unaweza kushangaa mtu ambaye alikuwa na upeo wa hali ya juu anaweza kuanza kufanya kama ana fikiri kwa kutumia masaburi.
Kuwa Kiongozi haikufanyi upoteze the social part of yourself. Nani amekwambia kwamba ukiwa kiongozi ndo usinywe pombe na wanakijiji wenzio? Cha msingi hapa ni kuwaelekeza wajue muda gani wa kunywa pombe na muda gani wa kufanya kazi. Tusipende kuishi maisha ya kuigiza (artificial life) eti kwa vile wewe ni kiongozi ndo usinywe na kufurahia kinywaji na wananchi.....
Mtu ni afya haya ni mambo ya kale sana
Hii ni dalili ya Utumwa.Ukiona hivi jua anaetuhumu hana asilia,hakika Pinda japo kuna ambayo amenichefua nayo ila kwa hili,umenionyesha kuwa bado ujamezwa na ukoloni mambo leo.Be proud of your origin.Asiyekubali asili yake jua huyo ni mtumwa.Viongozi wengi ndani ya Taifa hili ni Watumwa kupindukia.
Wakishajua kuvaa suti na mashari ya Mark Spenser basi wanasahau mila na desturi za vijijini kwao na pombe zilizowalea wanaziona kinyaa,ni aibu kubwa sana.Ukiona mtu anakandia au zodoa mila na utamaduni [Cultural and Traditional] jua huyo hana kwao.Kikwetu tunasema LA WILELO.Yaani huyu hana asili yupo yupo, hajui A wala BE,yaani ni MFU.Kesho uchumi wa dunia ukisambaratika kwa maana ya kiwanda cha bia kufungwa kwa kushindwa kujiendesha Mtanzania wa asilia ambae amesoma na anaheshimu mila na desturi yake ataludi kwenye pombe yake ya asilia na kuendelea na maisha kama kawaida na sio mwisho wa maisha bali ni mwisho wa kiwanda cha kizungu [Civilization] na ajira ya wakati ya baadhi ya Watanzania wa sekta hiyo.
Katika makabila ambayo yana wasomi kwa maana ya watu waliostaarabika [Civilized] lakini wanapenda kutumia na kuendeleza Pombe yao ya ASILIA hata kama akichaguliwa kuwa UN SECRETARY bado atarudi kuinywa na kuagizia atengenezewe ni WACHAGA NA MBEGE au Mkurya na OBUSARA [TOGWA] au OBULANDI.
Hivyo Utumwa wako Kwa wengine ASILIA hawaichi,Mwenye ASILI JASILI.
semeni ha hii sasa