Pinda amfunza Makamu wa Rais unywaji pombe ya kifipa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amfunza Makamu wa Rais unywaji pombe ya kifipa

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Nov 27, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]  [​IMG]

  Serikali ya CCM kama ni usanii tu nimeikubali. Pinda huyo kamchukua mzenj kwenda kumfunza kufyonza kimpumu (mataputapu) kwa kutumia mirija (straw) kule kulyamba lya mfipa, kukatavi.

  Hapo hata ile ya kibuku haifui dafu maana straw inaingizwa ndani ya chungu kilichopikiwa pombe ili kupata kitu kamili, hakuna kinachopotea njiani.
   
 2. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  So what! Mababu zako walikuwa hawafanyi hivyo!. Angekuwa amekaa hapohapo,na watu haohao, anakunywa John Walker whisk na mrija ungemsifia!.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna jambo moja muhimu hapa kuelewa juu ya nafasi na mzingira ambayo kiongozi mkubwa kitaifa anatakiwa awe mfano si wa kutunza utamaduni tu ila kutoendekeza mambo ambayo hurudisha nyuma maendeleo.

  Kesho hao hao watashinda vilabuni kwa hoja kwamba mbona Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu wakifika tunawaadalia pombe na wanakunywa, iweje sisi? Busara ni jambo muhimu sana..

  Nimeongea mara kadhaa kuwa mwana CCM maana yake umechagua kupoteza mwelekeo sahihi wa kufikiri, na hatima yake ndio haya tunayoshuhudia sasa. Unaweza kushangaa mtu ambaye alikuwa na upeo wa hali ya juu anaweza kuanza kufanya kama ana fikiri kwa kutumia masaburi.
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,069
  Likes Received: 7,547
  Trophy Points: 280
  Duh! Pinda kilabuni panamtoa na kumpendeza kichizi.
  Anyway nakumbuka kuna miaka hii style ya unywaji wa kutumia kata ulipigwa marufuku kule Tukuyu, kwa kuwa haukuwa healthy, nashangaa hapa tena waziri mkuu na makamu wa rais ndiyo wanautumia.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri kudumisha mila lakini ni vizuri pia kuangalia ni mila gani zidumishwe ni zipi hazifai. Kwa mazingira tuliyonayo sasa unywaji pombe kwa mtindo huo ni hatari kwa afya! Mtu mwenye ugonjwa fulani wa kuambukiza akitema mate kupitia huo mrija wengine wote mko hatarini kuupata.

  The whole thing looks very unhygienic hata ukiangalia sura ya Makamu wa Rais ni wazi anashangaa watu wanakunywaje that thing? Hapa dhana ya maendeleo inakosa maana kabisa kwa kuangalia Waziri mkuu anafanya nini! Vikombe vimekosekana?
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkataa kwao Mtumwa.Its a nice thing I like our local Tanzania brew beer Kimpumu unashushia na kawimbo kazuri kutoka kwa kina mama ka "Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni."
   
 7. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hapo kimsingi nani boss wa mwingine ktk utekelezaji wa majukumu ya kitaifa yaani waziri mkuu na makamu wa rais kimadaraka nani kamzidi mwenzake.
   
 8. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hii ni dalili ya Utumwa.Ukiona hivi jua anaetuhumu hana asilia,hakika Pinda japo kuna ambayo amenichefua nayo ila kwa hili,umenionyesha kuwa bado ujamezwa na ukoloni mambo leo.Be proud of your origin.Asiyekubali asili yake jua huyo ni mtumwa.Viongozi wengi ndani ya Taifa hili ni Watumwa kupindukia.

  Wakishajua kuvaa suti na mashari ya Mark Spenser basi wanasahau mila na desturi za vijijini kwao na pombe zilizowalea wanaziona kinyaa,ni aibu kubwa sana.Ukiona mtu anakandia au zodoa mila na utamaduni [Cultural and Traditional] jua huyo hana kwao.Kikwetu tunasema LA WILELO.Yaani huyu hana asili yupo yupo, hajui A wala BE,yaani ni MFU.Kesho uchumi wa dunia ukisambaratika kwa maana ya kiwanda cha bia kufungwa kwa kushindwa kujiendesha Mtanzania wa asilia ambae amesoma na anaheshimu mila na desturi yake ataludi kwenye pombe yake ya asilia na kuendelea na maisha kama kawaida na sio mwisho wa maisha bali ni mwisho wa kiwanda cha kizungu [Civilization] na ajira ya wakati ya baadhi ya Watanzania wa sekta hiyo.

  Katika makabila ambayo yana wasomi kwa maana ya watu waliostaarabika [Civilized] lakini wanapenda kutumia na kuendeleza Pombe yao ya ASILIA hata kama akichaguliwa kuwa UN SECRETARY bado atarudi kuinywa na kuagizia atengenezewe ni WACHAGA NA MBEGE au Mkurya na OBUSARA [TOGWA] au OBULANDI.

  Hivyo Utumwa wako Kwa wengine ASILIA hawaichi,Mwenye ASILI JASILI.
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Pinda jicho limewiva!!!ameanza kulembua unachezea chimpumu na msabe!!chai ya pombe!!
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wako umetoka nje ya mtazamo wangu. Ukisoma maoni yangu sijadharau pombe, ila namna gani hiyo pombe inywewe na kwa nafasi gani. Mara kadhaa pombe hupikwa au kutayarishwa katika mazingira yasiyofaa kiafya. Hali kadhalika njia au utaratibu unaotumiwa kunywa pombe si bora kwa afya kama mmoja livyopendekeza hapo juu. Ni hatari kwa kuambukizana magonjwa kwa kushirikishana vyombo tuvitumiavyo wakati wa unywaji.

  Pia katika nafasi hiyo hali ilivyo Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wanahamasisha ulevi kwa wananchi, hilo si jambo la kukingia kifua, na si dhana nzuri kwa viongozi wa taifa kufanya jambo kama hilo hadharani kwa kila walifanyalo hunukuliwa na kutangazwa katika kadamnasi na kutujuza namna fikra za viongozi wetu zilivyo. Kuna viongozi wetu kadhaa huvuta sigara lakini ni jambo binafsi ambalo hawalionyeshi hadharani kwa vile si jambo la kufunza umma. Viongozi kadhaa wana vimada, lakini ni siri yao, vinginevyo wakionyesha hadharani si jambo la kukubalika kijamii. Haya mambo wangeyafanya huko walikofikia baada ya kumaliza shughuli zao, lakini unywaji pombe kwa kushirikisha chombo kimoja hadhari na kwa nafasi walizo nazo si jambo la kufumbia macho, wameteleza.

  Sehemu nyingi nchini utumiaji wa vifaa vya kiasili katika unywaji pombe vilishapigwa marufuku, kama kutumia vibuyu kwani huwezi ona nini kimo ndani ya kibuyu. Hali kadhalika sharing ya vyombo wa kunywea ni hatari mno kwa afya kuambukizana magonjwa. Mimi mwenyewe ningali mdogo na kuanza kupata akili nilikuwa na mtazamo tofauti hata kabla sijaenda shule, na akili ilipopevuka nilifurahia uamuzi wangu wa awali wa kulinda afya yangu kwani ni ukombozi uliotukuka.

  Nilipinga na kukataa kata kata kuchanjwa usoni na kwa bahati nzuri wazazi wangu waliheshimu uamuzi wangu, vinginevyo leo ningekuwa na makovu ya kuchanjwa usoni eti kwa vile ni utamaduni tuliorithi toka kwa wazee wetu.

  Hayati Tumtemeke Sanga alitetea zao la bangi liendelee Jimboni kwake Makete wakati akichangia hoja bungeni, pamoja na kwamba wananchi wa jimboni mwake hawakuwa wanatumia bangi kama kileo bali kama kiungo kwenye mboga za majani na mabua yake kutoa kamba nzuri za kushona mikeka, hoja yake haikukubalika kwa sababu ya athari ambazo wengi wanaathirika kutokana na utumiaji wa bangi. Hata mimi udogoni nimeona zao la bangi likilimwa na kutumiwa, lakini leo siwezi kupigia mbiu zao la bangi maana jamii kubwa inaathirika kutokana na matumizi yake.

  Utetezi wako umepwaya mno kwa kutetea utamaduni tu bila kuangalia athari zake kwa jamii hiyo hiyo inayoendekeza unywaji wa aina hiyo. Mazuri ya utamaduni tunayenzi, lakini kutetea unywaji huu ni sawa na kujiunga na wanaotumia kufikiri kwa viungo visivyoasiliwa kwa kazi ya kufikiri.
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  usiku wake alimfundisha kula kiti fire
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Makamu wa rais akiwa katika dini yake kuwepo katika jopo la kutumia pombe kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya dini yake anawafunza vipi waumini wake? Unaweza amini nisemayo ukiwa CCM uwezo wa kufikiri na kupima mambo hata kwa akili ya kawaida hupungua?

  Waumini wa dini ya kiislamu watamwelewaje Makamu wa Rais? Visiwani kuona picha hiyo wanabaki kushangaa yaliyojilia hata ajiunge na jopo hilo ya kutumia alcohol kwa kushirikiana kuvyoza kutumia mrija (straw) [lupembechu] atajiteteaje?
   
 13. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45

  hivi wazanzibari hawanywi pombe kabisa?
   
 14. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Nafasi (post) ya Umakamu wa Rais ni taasisi; gaina dini wala kabila. Ndio maana anaalikwa shughuli za kidini, kikabila,nk!

  Hakanywa KIMPUMU anayokunywa PM; anachofanya ni kushuhudia! Kosa liko wapi?

  Akiemda kukagua miradi ya kilimo na ikatokea ktk moja ya farms kuna nguruwe hatokwenda?

  Wacheni kuendekeza udini hata kwenye kujisaidia msalani!
   
 15. driller

  driller JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 1,119
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  ila nasikia mzee kwa mambo ya bar ni mzima kweli kweli jamaa
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  Kuna mirija mitatu ya kufyonza pombe pale, moja ya Pinda, moja ya yule mama na nyingine ya Makamu wa Rais, usipindishe habari, kwani kesho tukikukuta upo unavinjari eneo la machangudoa maana yake unafanyia mahesabu ya kuwapata.

  Na huo mtungi kuna siri ile ya maana ya kusumbawanga na maana yake ukitaka kujua nenda pale Mazwi watakueleza maana ya wanga, kule mji mwema mchanganyiko hawajui maana ya sumbuwanga. Ukidharau na kuendelea na safari baada ya kuvuka gati la wanyamapori la Katavi gari likigoma kupanda mlima wa Lyamba lya Mfipa usijejutia.

  Kuhalalisha hilo ipo siku ataenda kukagua mashamba na kukuta bangi ikitumiwa na wakinga kama kiungo cha mboga za majani na kushiriki itakuwa ni busara zaidi? Maana cheo si kinga ya uvunjaji wa taratibu za mila, afya na kanuni.
   
 17. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,877
  Trophy Points: 280
  Hakuishia kujifunza tu, bali naye alikunywa hadi akazuiwa na PM mwenyewe!
   
 18. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  UCHUMI WA TANZANIA UMESHUKA NA TANZANIA IKO HATARINI KUFILISIKA BADALA HAWA VIONGOZI WAKUBWA SERIKALINI WAKAE WAJADILIANE JINSI YA KUIOKOA TANZAnIA WAO WANAPOTEZA MDA KUFUNDISHANA UNYWAJI WA MAJI TAKA!!
   
 19. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hata bia ni maji taka
   
 20. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sababu ya tanganyika kuendelea na muungano wa zanzibar ndo kama hii kudumisha mila na desturi za kibantu na kuondokana na ule ukiritimba wa kimanga wanaofanyiwa wabantu wenzetu huko visiwani
   
Loading...