Tunashukuru kwa picha. Ni tumaini letu kwamba baadaye itawezekana kuziweka hizo picha zionekane kwa urahisi, kama zilivyoonekana picha za Arusha.
Tunaomba HOTUBA ya Dr. Slaa huko Rombo vile vile. Watanzania wengi tuna kiu ya kumsikiliza Dr. Slaa wakati huu. Tunategemea ndiye mtu wa kutupeleka kwenye AWAMU YA PILI YA UHURU wetu. AWAMU YA KWANZA ilikuwa 1961 - 2010. TANU na CCM ndio vyama vilivyoongoza nchi wakati wa awamu ya kwanza. UKOLONI MAMBOLEO uliigubika sana awamu ya kwanza. Inabidi kuanza miaka 50 mingine (AWAMU YA PILI) na viongozi wengine.