Pepsi na magari yao

Cheusi Dawa

New Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
2
Reaction score
1
Nitangulie kusema ni umbea tuuuuuuuuuu
Ila napenda kujua if baadhi ya company yanaruhusu magari zao kuendeshwa na watu wasiohusika moja kwa moja na ma -company hayo.

Kuna mdada m1 mfanyakazi wa PEPSI, hapo Ilala Bungoni karibu na GAlapo - club Masai (DSM), anadrive gari la PEPSI aina ya Nissan jeupe (dabo kebin). Huyu mdada ana mmewe ambaye nilipata kumfahamu miaka mi2 iliyopita baada ya kutaka kuniuzia gari lake 1. Huyu bwana huwa anadrive hilo gari mtaani hapo siku za wikiendi na jioni/usiku.na kuwadanganya baadhi ya watu (wasio mjua) kuwa yeye ni mfanyakazi wa pepsi (labda kwa kuwa waliambiwa wamekuwa mwili m1 na mkewe).

Nilitakan tu kujua kama baadhi ya company unaruhusiwa kutumia gari na familia yako? maana hapa kwa mwajiri wangu, gari hata staff kama hajakabidhiwa haruhusiwi hata kulisogeza.

Ni umbea tuuuuu

CD
 
..Nilitakan tu kujua kama baadhi ya company unaruhusiwa kutumia gari na familia yako? maana hapa kwa mwajiri wangu, gari hata staff kama hajakabidhiwa haruhusiwi hata kulisogeza.

Ni umbea tuuuuu

CD
Ndio kuna makampuni yana sera ambazo hazikatazi ('zinazoruhusu'!) hilo (hasa kama ni gari la kutembelea) provided unayempa gari aendeshe anayo valid driving licence.
 

huo kweli umbea,na ummbea kweli roho inakuuma kwa mali za wahindi wakati maliza za taifa lako zinaliwa na mafisadi wala huoni uchungu umekalia umbea tu. Kuna magari mangapi ya serkali yanajivinjari usiku wa manane na watoto wa vigogo? Kuwa mvumilivu acha roho ya kwanini na umbea
 
CD, kweli wewe ni mbeya, hata hivyo ni post yako ya kwanza baada ya kuwa umejiunga JF leo. Karibu ila punguza umbea.
 
Utasutwa wewe hapa oho....ww si mgeni?punguza umbeya
 
Kawaulize hao watu wa PEPSI kuhusu magari yao
 
Hii ina sehemu yake sio hapa ,kuna forum ya udaku/utani
Peleka kule
 
Hayatuhusu. Umbeya tu. Anzisha mada yenye mantiki. Kwa mawazo yako, unaona hii ni mada kweli?
 

utasutwa shauri yako
 
Hiloooo, umbea kwenye mali za wahindi. Kweli wewe abunuasi. Leta umbewa wa nyara za taifa ambazo zinakuhusu moja kwa moja
 
Hiloooo, umbea kwenye mali za wahindi. Kweli wewe abunuasi. Leta umbewa wa nyara za taifa ambazo zinakuhusu moja kwa moja
Ni kweli kuwa mali za serikali zinaibiwa, lakini kwani kuna ulazima wa kuwataja wahindi? Kwani hao wahindi sio watu? nusu ya wanaofanya kazi za viwanda nchi hii wameajiriwa na hao wahindi lakini choyo tu, kila kitu kama si wahindi ni waarabu, utafikiri hizo Bhesco na Hosco na Aisco na Gapex wamezimaliza wao, pole pole jamani
 
Ndio kuna makampuni yana sera ambazo hazikatazi ('zinazoruhusu'!) hilo (hasa kama ni gari la kutembelea) provided unayempa gari aendeshe anayo valid driving licence.

Nashukuru SMU kwa ufafanuzi wako. Nimeelewa tofauti zilizopo kwenye ma-company. Nia yangu ilikuwa hiyo tu na nadhani nimepata point ya kuweza kuwashawishi waajiri wangu walegeze hizi taratibu.
ubarikiwe
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…