Penzi jipya la kero....

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,475
Reaction score
21,046
"Baby Umeamkaje Baby umekunywa Chai,Baby umevaa lile shati nililokununulia,Baby umepiga viatu kiwi,Baby umefika kazini,Baby mbona kimya,Baby hujanimiss eh,Baby mchana utakula nini,Baby umekula,Baby hebu nipigie picha chakula chako unitag,baby niko Mwenge naenda kutengeneza kucha,Baby nimeona vipochi vizuri hapa Makumbusho utanileta eh,Baby unatoka saa ngapi,Baby nitakuona leo,Baby duuuuuuhhhh... Kuanzia Asubuhi umeamka hadi jioni unaitwa BABY mara 76...Na anataka message zote umjibu,usipomjibu ananuna kama mtoto aliyenyimwa Ubuyu mwekundu...Hapo bado simu zake upokee,hasira zake za message za bure za CHEKA NAO anamalizia kwako...JAMANI TUTAFANYA KAZI KWELI????Kila muda Baby kweli,mwishowe ipo siku tutamuita Bosi Baby sasa maaana ndo jina liko mdomoni kila saa...Chezea penzi jipya wewe,Full Vibration kama Nokia Asha! Kwa Hisani ya Wanawake woteeee walio dimbwini kimahaba..
 

WIZI mtupu hakuna jipya na bado utamalizwa na vilio na makelele kitandani basi unajiona bonge la BEIBE..........!
 
Utakua umekutana na mtoto wa kike siyo mwanamke
 
Usipopendwa unalalamika, ukipendwa unalalamika, tukueleweje?
Mapenzi ya hivyo ni mazuri sana iwapo anayependwa anakuwa na akili timamu. Ipo namna ya kumtuliza, waweza kumdanganya kwamba niko kwenye kikao - tuwasiliane jioni, inatosha.
 

Utaitweje baby? wakati wewe mtu mzima na ndevu zako,Ukiona hivyo mkuu ujue hapo ni usanii mtupu.
 
hivi shule zinafunguliwa lini vile ?
 
nafikiri wangu ni mwanaume mwenye bahati sana duniani.hakuwahi kukumbana na hiyo karaha toka uchumba hadi ndoa.
 
Mimi huwa nasema Amini nakupenda kwa dhati kutoka moyoni.Baby zinaweza zikawa nyingi halafu fake!Elewa nakupenda kwa dhati si lazima nikuletee ua zuri la thamani halafu nikawa na penzi fake.Kuna watu wameendekeza starehe ili kuwaridhisha wapenzi wao mwisho wa siku wameishia kuishi maisha ya shida kiuchumi na kiafya pia.Wanabaki kusimulia enzi zangu nilikuwa natesa swali je kwa sasa una nini cha kujivunia kimaisha?Fanya kazi kwa bidii na ujue kila fedha unayoipata utumie vyema hujui baadaye na watoto wanakuja pia.baby baby nyingi bila kufanya kazi si nzuri.
 
nafikiri wangu ni mwanaume mwenye bahati sana duniani.hakuwahi kukumbana na hiyo karaha toka uchumba hadi ndoa.

Inawezekana kuna ukweli ndani yake maana wanawake wa namna hiyo wapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…