Wakuu,
Kwakuwa suala la kuwakilisha wananchi sio la mtu mmoja, na wenye sifa ni wengi hasa kati zama hizi ambazo wasomi ni wengi,
Kwakuwa matatizo ya jimbo husika yanajulikana hivyo sio kwamba mtu mmoja ndo mwenye upeo wa kuyaona,
Kwakuwa mbunge analipwa mshahara, mwisho wa kipindi chake anaweza lazimishwa kutoa taarifa ya mahali alipoishia na wapi dira ya jimbo inaelekea,
Kwakuwa serikali yetu ni ya kijamaa, na katika ujamaa watu wote ni sawa,
Napendekeza wabunge wawakilishe miaka mitano kisha wawaachie wengine.
Mtu anaongoza jimbo moja miaka ishirini hali ya kuwa kuna watu wengi jimboni wenye sifa kama zake au zaidi inakuwa sio sawa.
Inatokea mpaka mtu anaamini jimbo ni mali yake, hata akishindwa hakubali kirahisi.
Kama inatokea mbunge ana upekee, baada ya miaka mitano aingie kwenye zile teuzi 10 za rais. Ili kufanikisha hili wanaweza ondoa zile nafasi za viti maalumu ambazo nazo zimelalamikiwa sana hasa kwa namna wale watu wanapatika na 'impact' yao wakishazipata zile nafasi.
Karibu kwa maoni