Kila kitu Warioba tu, tunahitaji na wengine waseme!Ndg. wanajamii kutokana na hali ya mkanganyiko wa sasa wa mchakato wa Katiba, napendekeza kuwe na mdahalo ambao wazungumzaji wakuu wawe:
1. Jaji Joseph Warioba
2. Prof. Kabudi
3. Mh. Samweli Sita
4. Mh. Andrew Chenge
Mdahalo huu utangazwe na vyombo vyote vya habari binafsi na vya serikali.
Washiriki wawe wahariri vyombo vya habari ili kupunguza zomea zomea na kutupa fursa wananchi kuchambua mbivu na mbichi.
Nawakilisha.
Raia wa kawaida nisiye na upande.
Kila kitu Warioba tu, tunahitaji na wengine waseme!
Napemdekeza pia awepo Prof Issah G. Shivji!Hayo ni mawazo yangu finyu, si vibaya ukipendekeza wasemaji wengine natumaini taasisi zitakazojitokeza kuandaa mdahalo huu watawafikiria.
Napemdekeza pia awepo Prof Issah G. Shivji!
Ahsante si wazo baya cha msingi, wananchi tupate ukweli toka kila upande ili tufanye maamuzi sahihi,
Napemdekeza pia awepo Prof Issah G. Shivji!
Iliyokiwa Tume iko biased sana, wajumbe wake wakiwa wengi tutapata mawazo ya upande mmoja!Wazo zuri ila hao namba 3 na 4 hawawezi kukubali. Na upande wa Zanzibar nako kuna wataalamu wa katiba wawepo wawili, mmoja toka kwenye tume na mmoja toka BMK masalia.