Kwa katiba yetu hiii mpya, ningependekeza kuwa na kipengele cha kunyongwa marais, mawaziri, makatibu wakuu, mameneja kwenye taasisi za serikali, na wabunge mara wakibainika na wizi madarakani ama kula rushwa. Kuwe na kipengele cha rais kushitakiwa na kufukuzwa kazi kwa manufaa ya umma pindi akipatikana na hatia ya ufujaji madaraka na wizi. Hii katiba ianze kuchunguza marais wote toka enzi za Mwinyi mpaka hapa tulipofikia. Kwa kifupi, rais awe kwenye mikono na macho ya watu waliomuweka madarakani na asiwe kama dikteta. Tuwe na mfumo kama marekani ama nchi nyingine zilizo endelea.