Wadau nina tatizo na Laptop yangu ina zingua sana inakuwa inazima na kujiwasha na kisha inaleta blue screen na maandishi mengi sna kisha ikitulia inafanya kazi wakat mwingine inaleta mistari kwenye screen hasa napoanza kuplay video yoyote ile. mtaalamu yeyote anisadie.View attachment 84496
Cheki mkanda unaounganisha screen na laptop bottom(ehemu inayokaa mezani)..Mara nyingi huwa mkada ukiwa umelegea au umekatika inakua kama ina piga dim dim hivi wakati wa kuwaka....
Kama sio tatizo basi jaribu kucheki VIDEO CARD au GRAPHICS CARD in tatizo..Ila sio shida ya software ni hardware failure
Screen haina taizo kabisa wala huo mkanda, kwani kuna wakati inaniandikia display not.....ila hasa kuna driver inaitwa NVIDIA GEFORCE 8400M GT yenyewe haina tatizo tazizo ni hardware ya hiyo nvidia ndo maana nikahitaji mtaalamu anaeweza anisaidie
Kwa haraka haraka nakushauri tafuta fundi au angalia yafuatayo:-
1. Check na RAM kutokana na vumbi na joto yawezekana ilaleta tatizo hilo.
2. Kama iliwahi kuhanguka basi kuna uwezekano wa cables na baadhi ya vijipande vya chuma kugusa circuit na ku-short.
3. Tafuta External monitor na test kama symptom unayoipata ni hiyo hiyo ya mistari.kama lah basi monitor ishafika kwao ilipotoka.Nawakilisha
Mr. clajago ahsante kwa ushauri wako ila hivyo vote nimeangalia na kubadilisha na kuweka vipya mpaka hard disk nayo nilibadili, pamoja na kutafuta monitor nyngne tatizo lipo ndani wala sio hivo vitu ulivovisema.