Pc inanizingua naombeni msaada

DEVUQUARTER-DEVUKOTA

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
352
Reaction score
117
Wakuu laptop yangu ya toshiba imeanza kunizingua display yaani ukiiwasha inawaka fresh ila tatizo kwenye display hakuna mwanga kabisa so naona kwa taabu maana giza tupu.
Nimejaribu option ya kupandisha mwanga kwa kubonyeza zile buton za fn na zakupandisha mwanga but bila bila.
Magwiji wa haya madude niokoeni tafadhali
 
Tia kwenye ndoo ya maji baridi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

jaribu ku-adjust mwanga kwa kutumia Windows Mobility Center kama unatumia windows 7 au 8) kwa kubonyeza WinKey + X au nenda kwenye contro panel tafuta power options then jaribu kumodify kutokea huko
 
Mkuu Nyasiro mbona umebadilisha avatar yako?ya zamani ilikuwa nzuri kuliko ya sasa au hutaki watu wakufahamu nini?
 
jaribu ku-adjust mwanga kwa kutumia Windows Mobility Center kama unatumia windows 7 au 8) kwa kubonyeza WinKey + X au nenda kwenye contro panel tafuta power options then jaribu kumodify kutokea huko
Nikifika home nitajaribu mkuu maana niliona mzigo kulibeba
 
inaonekana ni BONGE ya laptop mpaka umeona mzigo kuibeba
Dude linasumbua sasa la kazi gani kuzunguka nalo?
Ajabu nilipofika home iliwaka fresh kabisa bila ya kutumia theory ulizonipa ila baada da dk 15 ikarudi kama mwanzo.
Nimejaribu hizo njia zako Kamanda but hakuna effect yoyote yaani kizungu zungu tupu mpaka natamani kuibamiza
 
I have seen this problem caused by a slightly displaced lcd-display cable and also invertor.
When you move the screen away from you and back does it change or dim ?

 
Tia kwenye ndoo ya maji baridi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mbona wengi tu hawajui jinsi ya kumsaidia hy jamaa kama na wewe pia hujui ni vema ukatulia tu kuliko kuwakwaza watu humu ndani.
 
Nawashukuru wadau wote walionichangia huu uzi Nyasiro ALEYN shukrani za pekee kwako bs0d coz mchango wako ndiyo umenisaidia maana nilipojaribu kuifungua display kucheck vizuri nimekuta screw inagusanisha nyaya kwenye surface ya invertor baada ya kuiondoa hiyo screw na kuifunga upya display sasa pc ipo fresh tatizo out.
Ila sijajua ile screw imefikaje kule maana tokea ninunue ndiyo kwanza naifungua.
 

Krapika davinoooooooooooo nakusalimu 2
 

ilishawah kunitokea, je ukibonyeza ctrl+alt+del ikaja task manager ukaenda new task na kurun programs na mafile yanaonekana? Meaning screen yako ni nyeus bt cursor pekee ndo yaonekana? Obvious kana ni hvyo mie nilibackup vitu vyangu nikapiga window chini..
 
@ Devuquarter;
Aisee kwa fundi wa kawaida Dar... unge acha angalau Hamsini elfu na baada ya uzushi mwingi!
 
@ Devuquarter;
Aisee kwa fundi wa kawaida Dar... unge acha angalau Hamsini elfu na baada ya uzushi mwingi!
ushapigwa changa la mdomo so hupati hata ya soda.
Davinoooo ebunjoo unaitwa huku
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…