kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,685
Pato la Mtanzania limeongezeka kutoka Sh. milioni 869,436 mwaka 2011 hadi kufikia Sh. 995,298 mwaka jana, Bunge limeelezwa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2013/14. Alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 12.6 na pia alitaja kuwa Pato la Taifa nalo limeongezeka kutoka asilimia 6.4 mwaka 2011 na kufikia asilimia 6.9 mwaka jana, huku mfumuko wa bei ukishuka kutoka asilimia 19.4 hadi asilimia 10.4 Februari mwaka huu.
"Kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na jitihada za serikali za kuongeza usambazaji wa chakula kwenye masoko, kupunguza ujazi wa fedha kwenye soko, kudhibiti upandaji wa bei ya mafuta ya mitambo na kuimarisha upatikanaji wa umeme viwandani ikilinganishwa na mwaka 2011/2012."
MAUAJI YA WAZEE, ALBINO
Waziri Mkuu amesema kuwa kuibuka upya kwa mauaji na ukatili dhidi ya wazee, wanawake na walemavu wa ngozi kwa katika baadhi ya mikoa kwa sababu za kishirikina, kunaharibu sifa ya taifa.
"Ukatili huu siyo tu unyama uliopindukia kwa binadamu wenzetu, bali pia unaondoa sifa kubwa kwa jamii yetu ya kupendana pasipo kujali rangi, kabila wala dini," alisema.
"Nitumie fursa hii kuwahakikishia albino, wanawake na wazee kwamba serikali haitavumilia kuona ukatili wowote unafanywa dhidi yao, naziagiza kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kushirikiana na wananchi kuwabaini na kuwafikisha kwenye sharia wanaojihusisha na vitendo hivi," aliongeza.
MIGOGORO YA DINI
Waziri Mkuu Pinda alisema hivi karibuni kumejitokeza migongano na chokochoko za kidini ambazo zimeanza kueneza chuki miongoni mwa Watanzania na kwamba si dalili nzuri za mustakabali wa nchiinayopenda kudumisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
"Uzoefu wa mataifa mbalimbali umeonyesha kwamba chokochoko za kidini zimesababisha machafuko makubwa na kutoweka kwa amani. Tukumbuke yakitokea machafuko ya namna hiyo na kuvuruga amani na utulivu hakuna atakayesalimika," alisema.
Aliwataka viongozi wa dini kuthamini na kuheshimu dini za wenzao na kuepusha vitendo vinavyo amsha chuki miongoni mwa waumini wao.
WAKULIMA KUFIDIWA
Waziri Mkuu aliliambia Bunge kuwa serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha mfuko maalumu wa kufidia bei za mazao pale zinaposhuka lengo ni kuwawezesha wakulima kupata bei nzuri na kuwaepusha na hasara zinazotokana na kushuka kwa bei za mazao katika masoko ya kimataifa. Kadhalika itawahamasisha kuendelea kulima mazao yao.
Alisema hatua hiyo inalenga pia kudhibiti mwenendo wa bei za mazao makuu kama pamba, kahawa, chai, tumbaku, korosho, katani na pareto ambayo hubadilika. Waziri Mkuu aliomba Bunge kuidhinisha Sh. trilioni 4.226 za ofisi yake na Sh. Bilioni 123.4 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
SEKONDARI 264 KUJENGWA
Shilingi bilioni 56 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari 264 nchini.
Hayo yamo katika maelezo ya kiutendaji yaliyotolewa bungeni jana na Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia kuhusu mapitio ya kazi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na mwelekeo wa kazi kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Alisema katika awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya sekondari kwa mwaka 2012 hadi 2014, Serikali imelenga kujenga shule mbili katika kila halmashauri.
Alisema shule hizo zitawekewa mahitaji muhimu kama madarasa, nyumba za walimu, maabara, vyoo, maji na samani.
Alisema uteuzi wa ujenzi wa shule hizo umeshafanywa na mamlaka za zabuni za serikali za mitaa.
"Halmashauri zimetangaza zabuni na wazabuni walioshinda wapo katika hatua ya kuingia mikataba ili kuanza kazi ya ujenzi," alisema. Kuhusu fedha za chenji za rada kutoka kampuni ya BAE System, alisema kiasi cha fedha kimeongezeka kutokana na kupanda kwa thamani ya fedha na riba ya benki hadi kufikia Sh. 78,718,180,000.
Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo, fedha za ununuzi wa vitabu imefikia Sh. bilioni 59,038,635,000 na fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati imefikia Sh. 19,679,545,000.
Ghasia alisema Kamati Endeshi ya matumizi ya fedha za BAE System iliamuliwa kuwa aina ya dawati liwe ni la kukaliwa na mwanafunzi mmoja.
"Hii inatokana na kuhama katika mfumo wa ufundishaji na kuwa mfumo shirikishi ambapo wanafunzi wanajifunza kwa kujadiliana zaidi na kuchangia mawazo ya uelewa wao kuliko kumsikiliza mwalimu," alisema.
Ghasia alisema baada ya uchaguzi wa aina za madawati yatakayonunuliwa na kupata viwango vya madawati hayo kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, zabuni zinatarajiwa kutangazwa mapema mwezi huu.
Hata hivyo, alisema kutokana na maamuzi ya Bunge la bajeti la mwaka huu (2012/2013), liliazimia kuwa madawati yanunuliwe na kusambazwa katika halmashauri zote nchini badala ya halmashauri tisa tu.
Kuhusu vitabu vitakavyonuliwa kutokana na fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya vitabu, Ghasia alisema mchakato kwa ajili ya ununuzi wa vitabu umekamilika na serikali imeingia mkataba na wachapishaji tisa wa vitabu pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania ambayo inajukumu la kuchapisha mihtasari na miongozo yote. "Kulingana na mkataba kazi hii imetengewa miezi sita kukamilika tangu kuwekwa kwa sahihi ya mikataba Machi 18 mwaka huu,"alisema.
Kwa mujibu wa Ghasia, serikali ilipokea fedha zilizotokana na fidia ya rada, Paundi za Uingereza 29,000,000 sawa na Sh. 73,6660,000 ambazo asilimia 75 kati yake zitatumika kununua vitabu vya kiada, kiongozi cha mwalimu, mihtasari na miongozo ya mihtasari kwa ajili ya shule za msingi Tanzania Bara.
Asilimia 25 zilikubalika kununulia madawati katika shule za msingi.
Imeandikwa na Gaudensia Mngumi na Sharon Sauwa, Dodoma
CHANZO – NIPASHE: Home