Habari zenu ndugu zangu wa JF
Nazani mtakumbuka mara ya mwisho kama sio wiki iliyopita nilileta hapa uzi wa public toilets kuwa na gharama kubwa sana hususani pale kituo cha daladala Mbezi mwisho, ambako hata kukojoa na kutema mate unatozwa 500/=,hali imekuwa tofauti katika kituo cha daladala cha mawasiliano ambako huduma zote mpaka kuoga ni 300/= tena cha kushangaza yaani mpaka dust bin lipo kwa bei ya 300/= tu.
Tunaomba serikali iifanyiekazi hii taarifa na iweze kutusaidia kwani pesa kwa sasa imekuwa ngumu, kukojoa uchovjoroni na kwenye machupa kuna wengine hatuwezi.