Shukrani kwa kutuhamasisha Bwana mazingira,umenifanya nitafakari mengi.wakati nasoma shule ya primary kipindi hicho ilikuwa ndio inaanzishwa 2003 .Kulikuwa Hakuna mti hata mmoja eneo la shule.wazazi na walimu wakakubaliana wachangie shilingi 20 kwa Kila mwanafunzi ili inununliwe miti na ipandwe Kila mwanafunzi alipewa kazi ya kuimwagilia Sasa ni 2019.miti hiyo ikiiona Leo hii imekuwa mikubwa Sana.Imesaidia kuleta kivuli,kupendezesha mazingira na hewa Safi.Pia wanafunzi wa Sasa wanafahidi juhudi za waliotangulia.
*Miti ina faida nyingi Sana hutupatia mbao,hutupatia kivuli,husaidia kuleta mvua,hutupatia matunda,kuzalisha hewa,pia hupunguza ongezeko la joto duniani linalozalishwa na shughuri za viwandani.Pia huzuia tabaka la ozone lisiyeyuke.Kuongezeka kwa joto husababisha maji ya bahari yaongezeke,hii inatokana na bara la Antaktika ambalo ni barafu huanza kuyeyuka kidogokidogo.Bara la Antaktika Hakuna kiumbe chochote kinachoishi ni barafu tu.misitu Kama Amazon ulioko nchini Brazil bara la South America na msitu wa Congo ulioko bara la Africa miti yake huzalisha kiwango kikubwa Cha hewa ya oksijeni duniani.Matumizi ya miti hayakwepeki ukikata mti usisahau kupanda mwengine hii itasaidia kunusuru nchi kukumbwa na desert.
#Kuwa mzalendo ipende nchi yako.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika