Siku za karibuni tulisikia upasuaji uliofanyika Hospitali ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya Moyo kwa mtoto kuweka kifaa cha bandia ndani ya Moyo Wake.
Je, Pacemaker ni nini? Moyo umeundwa na kitu kina kinachoitwa #SINOATRIAL NODE ambacho kazi yake ni kuzalisha umeme ili kusaidia moyo kusukuma Damu vizuri kwa mapigo yanayotakiwa sehemu za mwili.
Sinoatrialnode ipo chumba/chamber ya juu upande wa kulia (right atrium) wa moyo, sinoatrialnode ni pacemaker ya asili ya moyo(natural).
Endapo pacemaker ya asili inashindwa kufanya kazi kutokana na magojwa ya moyo ndipo pacemaker ya kutengenezwa (artificial) hupandikizwa katika moyo ili kusaidia Moyo kufanya kazi sawasawa kifaa hiki huzalisha umeme ambao husaidia moyo kusukuma damu hufanya kazi sawa na kile cha asili, kimeundwa na betri ambazo huweza badilishwa baada ya miaka 5-6 ukifanikiwa kukaa karibu na mtu mwenye hiki kifaa utasikia kikipiga kama mishale ya saa za ukutani pakiwa na utulivu na pale betri zinapoisha hubadilishwa na kifaa kuendelea na kazi zake hiyo ni Pacemaker.
Wataalamu tujuzane zaidi.