Kila mtu ananunua vitu , na ndipo hapa tunapata mahitaji yetu kama nguo , chakula nk. Zaidi ya hapo ni rahisi kununua vitu hovyo hovyo muda wote , hasa kipindi hichi cha online shopping (manunuzi kiganjani).
Kwa baadhi ya watu na kwa matatizo waliyo nayo, manunuzi yanageuka kuwa shuruti . nilitoa makala jana katika
forum JF,
reddit na
myexperinceproject,, naona wengi walitaka kujua nini hasa
compulsive buying disorder, ingawa wazungu wengi wanapenda kujua haya kuliko habari ya kulogwa na mapepo , ingawa ni mtembeo mmoja in different view .
ONIOMANIA...CBD (Compulsive buying disorder) ni ile hali ya kutojizuia kununua na kutumia muda mwingi ,pesa nyingi katika manunuzi. kununua vitu vingi pasina udhibiti ,, kumbuka huu ni ugonjwa au ni tatizo na ni tofauti na
overbuying ,, kwani mwingine ananunua vitu kwa sababu ana uhitaji , mwenye
CBD ni tofauti.
Mtu mwenye
CBD anasikia kutoka ndani ya moyo wake kununua (
strong desire) , awe na uhitaji hana uhitaji yeye anataka kununua tu , bila kufanya tathmini yeyote yaani anakuwa na
Negative emotion.
Katika ndoa mmoja wenu akiwa na
CBD lazima ndoa ife , kwani anakuwa analeta kitu kinaitwa ,,,
FINANCIAL HARM,, katika ndoa,,,, inahitaji mchungaji mwenye uelewa kutibu ndoa hiyo , unaweza kuwaza ni pepo kumbe ni tabia yako na pepo akakusindikiza tu
. Financial harm kifalsafa ndani ya ndoa ni sawa na mtu kuishi na maiti , lazima utakimbia tu ndani ya ndoa .
Mtu mwenye
CBD ( kununua kuliko kubuhu), kwa mujibu wa taasisi ya magonjwa ya akili ya amerika ( America psychiatric assosciation) pia anaweza kuwa na
HD (
hoarding disorder).
HOARDING DISORDER (tatizo la kuhodhi mali ) ni tatizo ambalo linaambatana sana na
CBD ni pale mtu ana nunua vitu na anagundua havihitaji vitu hivyo lakini pia hawezi kuviachia vikatoka mikononi mwake anapata shida kuvitupa au kugawia watu (
difficult parting with possesions). Unakuta mtu ana makorokoro mengi ndani ya nyumba na yote ana amini kuna siku yatamfaa.
Madhara makubwa ya
HD kwa mujibu wa tafiti ni uchafu na kwa nchi za ulaya wanaamini ni moto , kwani hayo mavitu yanaweza yakashika moto na kuleta madhara kwa haraka sana ,,, kwa marekani unakuwa umetenda kosa nafikiri unakuwa umefanya
health code violation ,,, na ndiyo maana uchafu mwingi sana unakuja Africa ……. Kwa sisi ukiwa na makoro koro unaonekana una vitu vingi ,,, kwangu nakuona una ugonjwa mkubwa sana wa akili.
Ni watu wa aina gani basi wanaweza kuwa ni wahanga wa manunuzi yaliyo kubuhu . mtu yeyote mwenye
negative emotion ( hisia hasi) ,,, yaani mtu
mwenye hasira , stress, maumivu,trauma, depression (mifadhaiko),kutojiamini( low self esteem), muoga nk.
Kwa ujumla wahanga wa
compulsive buying disorder ni wale wenye ugonjwa pia unaojulikana kama
BORDERLINE PERSONALITY DISORDER (BPD)( haiba yenye mashaka) … yaani ni ugonjwa wa akili , mtu anakuwa katika
mood swings , kuna wakati ana furaha , muda mwingine ana hasira , anacheka saa hiyo hiyo ana zira jambo , kususa nk . Anaweza akakufokea kwa jambo ambalo hukufanya .
Kwa mimi ni mtu wa kiroho siwezi kutokuhusia maandiko ya kitabu cha biblia . tunaishi katika dunia yenye dhambi
mwanzo 3:17-24, hivyo tuna madhaifu katika mwili na roho , kwa sababu tunaamini katika vitu zaidi kuliko Mungu , na ndiyo maana imeandikwa,,,
Mithali 3:5 “ mtumaini Bwana Mungu kwa moyo wako wote , wala usizitegemee akili zako mwenyewe . kuna mtu aliingia gharama yetu ya CBD ,, soma
2 wakorintho 5:21
Be inspired
kihiga@zoho.com