Ombi la kusaidiwa

Ninaomba kuendelea kuwaomba ndg zangu msisahau ombi langu
 
Habari za leo ndg yangu? Samahani. Ninaomba kama uliweza kufuatilia hili swala unieleze ulipofikia. Bado ninaomba unisaidie ngd yangu bado sijapata suluhu ya tatizo langu.
Asante.
 
Weka jina lako kamili,chuo unachosoma,registration number yako,course unayosoma,account number ya chuo na benk ya kulipia nikakulipia ada,utapata pay in slip utakayokwenda kubadilisha accounts na kupata receipts na kunipa feedback,simple like that!
Ndg Joowzey nilikutumia inbox details ulizohitaji. Sijapata feedback kutoka kwako. Ninaomba unipe taarifa za hatua uliyofikia. Bado sijapata suluhu ya tatizo langu ndio maana ninaendelea kuomba msaada wenu. Asante
 
Mambo kama haya yanaumiza sana,usijali utafanikiwa
 
Mwisho wa kulipa ada ni lini?
Mwisho ilikuwa tarehe 30/04/2018. Mpaka sasa nimepigwa fine kwa kuchelewa ngd. Ila ninaweza kulipa at least week moja kabla ya kuanza UE yaani tarehe 02-09 mwezi wa saba
 
Ndugu zangu ninaomba kuja tena kwenu kuwakumbusha juu ya ombi langu. Bado sijapata ufumbuzi wa tatizo linalonikabili na ambalo nilieleza kwa undani toka mwanzo. Wapo waliokuwa wameahidi kunisaidia kama ndugu Joowzey, Jiwe la majiwe n.k lakini kutokana na kutokuwa na mawasiliano yao mengine sina, inabidi niombe kuwakumbusha kupitia hapa. Siku zinazidi kuisha ndugu zangu na bado sijafanikisha kwa namna yoyote ile. Nawaomba msikie kilio changu. Asanteni.
 
Hili ombi ni genuine nenda katika mikutano ya hadhara ya Magufuli atakusaidia mkuu
 
Tatizo la JF bana, mtu unaweza kuwa very serious lakini watu wakaja na mambo yao ya utani. Mtu unaweza kuwa unaumia lakini watu wakaja na mambo yao yakebehi. "Jiwe la Majiwe" umejitutumua sana kwenye issue ya kumsaidia huyu kijana kisha umeingia mitini. Mambo mengine yanazidi kuumiza zaidi, ni bora ungakaa kimya na kuwa msomaji tu kama sisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…