Ombi kwa wakazi wa Dar mnaokwenda kusheherekea sikukuu na Weekend maeneo ya beach

Raskazimi

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
1,030
1,116
Kumbukeni mpo kwenye makazi ya watu. Mkikuta kuko kimya sio vibaya mkaheshimu ustaarabu huo, mambo ya kupiga muziki kwa sauti kwenye magari, bajaji na bodaboda zenu si ustaarabu.

Pia kuweni na heshima na barabara, pamoja na kuheshimu wanaokimbia na waenda kwa miguu. Pengine ni pombe au ujana, lakini spidi mnazoenda nazo na kuovertake ovyo mtaja kuua watu.
 
Naunga mkono hoja yako. Kuna tabia ya kutoheshimu uhuru wa watu wengine. Ipo tabia mbaya iliyozoeleka ya kuamua tu kufungulia mziki kwa sauti kubwa iwe kwenye mabasi, mitaani na baa zilizofunguliwa kwenye makazi ya watu. Kuna watu wakiona sehemu iliyoandaliwa vizuri mfano bustani binafsi, inageuzwa kuwa kijiwe au hata sehemu ya michezo bila kujali mmiliki ni nani. Tunahitaji kuwa wastaarabu hata bila kuigiza mambo ya kigeni.
 
uko daslam si mnasema wengine wanaishi uzunguni na wengine uswazi,
mtoa mada unaishi uswazi!
Lol!!
 
Back
Top Bottom