PostGE2025 Oktoba nilitiki kwa mbinde

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
9,129
Reaction score
22,875
Ila kutiki! πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜

Asubuhi ya October 29 nimeamka zangu nikawa na kiherehere mwenzenu, nikakimbilia kituo cha kupigia kura!

Wakati huo basi mambo shwari, nikawa najibaraguza pale napiga stori na makarani huku nikijifanya mimi ni usalama wa Taifa.

Mara paap, ma-genZ yakatuvamia, jamani tulibamizwa.... nilikimbia mpaka vishikizo vya shati vikakatika.

Magenz yalitufukuzia nyuma huku yanaturushia madumu ya kupigia kura. Sikumbuki nilichoropokea wapi nilijikuta niko ndani uvunguni.

Nimekoma kutiki.

Sitiki tena. Mnikome!
 
Wangekukata hata ka kidole 😏
 
Pole sana mkuu.
Kutik hakukatazwi ikiwa kura yako itathaminishwa na kutendewa haki kwa anayestahili ambaye ndiye chaguo lako.

Ipo siku tutapanga foleni zetu za haki na kutik kidemokrasia kwa viongozi tunaowapenda.

Umezitazama video zinazoonesha makarani wa uchaguzi wanavyoyatik maburunguru ya karatasi za kura na kuyashindilia kwa nguvu kwenye masanduku?

Ulipoteza muda wako bure.

'TIK TOK' yaani kutik ama kutoka ni uhuru na maamuzi ya mtu, ni demokrasia, ulitimiza wajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…