View attachment Poor school.bmp
Mazingira magumu haya ninyi viongozi mpo mnaishi kwa raha mstarehe, je ninyi ni watu mlioumbwa kama sisi mnaotuita masikini? Mh. Kinana juzijuzi ulipiga marufuku hili neno "MHESHIMIWA" Kwa makusudi mnatumia neno UMASIKINI katika majukwaa yenu bila kujua ATHARI ZAKE KWENU na kwetu. Neno hili ni sawa na Mzazi kumuita mwanae "Chausiku, Tabu, Logeni, Matatizo, Majuto, Wasiwasi, Mawazo, Nia gani, Sikudhani, Fitina na kadhalika" athari ya majina haya kwa mhusika mwenye jina ni kama yanavyosomeka,
Chausiku atakuwa hatulii kurudi kwake ni asubuhi yeye na wanaume tu,
Tabu yeye maisha yake yataakisi tabu iliyoko mbele yake,
Logeni yeye kila analofanya asipopata mafanikio atatangaza kalogwa,
Matatizo kama alivyo tabu yeye huyu atakuwa ni mtu mkorofi akipigana ovyo ovyo na wenzake,
Majuto atakuwa ni mnyonge kila mara kwa kutofanikiwa kwake,
Wasiwasi ni mtu atakaye ishi kwa hofu ya kutojua kesho atakula nini na mara nyingi hawa ndiyo wale tunaowakuta mitaani wakiwakaba watu kutatua shida zao. Sipendi kuendelea kuandika mengi kwani nitawafanya wasomaji wasipende kusoma mada ndefu.
Mnapotuita "WATU WA FAMILIA MASIKINI, JUENI YA KUWA NINYI NDIYO CHANZO HASA CHA KUTUFANYA TUWE HIVYO,
KUNA MSEMO UNAOSEMA ADUI YAKO MUOMBEE NJAA, SERIKALI ILI IENDELEE
KUTUTAWALA NA SI
KUTUONGOZA YENYEWE INASEMA "MWANANCHI ILI UWEZE KUMTAWALA MPE ELIMU MBOVU.
KUNA WAZIRI ANAITWA
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA UTAWALA BORA, FUTENI NENO
UTAWALA WEKA
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA UONGOZI BORA. MMEENDA HUKO KUTUTAWALA AMA KUTUONGOZA???
WAKOLONI WALIKUJA KUTUTAWALA NINYI BAADA YA UHURU HAMTUTAWALI BALI MNATUONGOZA TAFADHALI BADILIKENI KIFIKRA.
DO YOU WANT TO ASSURE US THAT YOU ARE AGENTS OF COLONIALISM???
please your party is ruling but you are leading us
PLEASE YOUR PARTY IS RULING BUT
YOU ARE NOT A RULER YET
YOU ARE A LEADER, LEADING US.
WHAT DOES A RULER DO? AND WHAT DOES A LEADER DO?
KWA NINI MNATUCHANGANYA HIVI.
TULIAMBIWA KUWA ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE
1. WATU
2. ARDHI
3. SIASA SAFI
4. UONGOZI BORA (SIYO UTAWALA BORA)