Oeni mabinti wa kisambaa mfurahie maisha

Shinbet18

JF-Expert Member
Jan 17, 2018
255
252
Habari za jioni wandugu wote humu ndani.Baada ya pilika zote za kutafuta mwenza wa maisha hatimae nimeangukia Kwa bint wa kisambaa kutoka Kauzeni Maramba Tanga.

Nilikotoka ilikuwa vita ya isiyoisha kila siku sitataja kabila la mke wa awali.Nilibanikwa roho ikauma kila sekunde mpaka nikadhoofu.

Baada ya kupata kimwana mweupe bila mkorogo umbo kama la Shunie nahisi kama kupaa.Mipango mingi iliyovurugika inarudi vema kila siku kama Christmas.

Bint ni mpole sio mkali mpaka namchokoza angalau aongee nione dimpoz za kisambaa macho yake goroli meno meupe yaliyo takaswa kwa maji ya milima ya usambara.

Naulizwa kama nataka kwenda kuoga ya moto au baridi ananisugua na brash la dodoki huko bafuni nafutwa maji na taulo linalonukia namwambia asante mke wangu.

Nachuliwa mgongo nirudipo safarini kabla ya kuandaliwa magimbi ya nazi niyapendayo sana.

Sitamaliza jamani sifa zake nimeona nishee nanyi raha nipatazo.
 
Hongera sana, na omba maisha yenu yaendelee kua na furaha. Jitahidi usimuudhi. Nilioa mtu wa kabila hilo, sina ham nae niliishi kwa dhiki ya nafsi na msongo wa mawazo. Siku nilioachananae ilikua ya furaha kuliko siku ya harusi yetu. Nilimuachia kila kitu pamoja na kiwanja tulichonunuanae. Sasa hiv nipo huru ila nataman mke kutoka Tanga.
 
tatizo linaanza baada ya miezi miwili ya ndoa,saizi anapiga debe kwa vile kuolewa inshu
 
Ni wakarimu sana, jiandae kisaikolojia...hawanyimi na uzalishaji mali jitahidi sana kwani huna msaidizi zaidi ya kufaidi kei
 
Back
Top Bottom