Hiyo kwa mwezi umeandika tu. Ukweli ni kwamba utataka kodi kwa mwaka 3,000,000/=.
Sheria ya nchi inasema kodi ya pango la nyumba ilipwe kwa mwezi (tena ambao mpangaji amekwisha kaa), nyie mnachukua ya mwaka (tena ulioko mbele ya kipindi ambacho mtu hajaishi kwenye nyumba). Matokeo yake mnawafanya watu wasiwe waaminifu makazini kwao.
Mjue tunapoendelea kutafuta mzizi hasa wa ongezeko la vitendo vya rushwa, ninyi wenye nyumba na tamaa zenu hamkwepi lawama katika hili.