Yupo mzungu alikua akiwachukia madalali. Basi, kila akipiga simu kuulizia property,anauliza swali; are the owner or an agent? Ukijibu wewe ni agent anakwambia no I want to deal withe owner. Basi mtandao wa matapeli ukainasa hiyo habari, wakajipanga mmoja akajifanya owner wakamchukulia huyo mzungu. Wakamchukulia kodi ya mwaka usd 8400. Matapeli wanawaogopa madalali sana unalijua hilo. Unajua asilimia 75 ya makaazi ya dar yapo katika maeneo yasiyopimwa. Sasa kama unataka kununua property kwa usalama nenda kaonane na madalali wa eneo hilo wao wanayajua maeneo hayo vizuri. Kinachokukela hapo labda hizo ada wanazokutoza kabla ya kwenda kukuonyesha property. Lakini mbona ukienda kwa mwanasheria kabla haujamuona anakutoza ada na aulalamiki? Au kwa sababu madalali wengi hawajakwenda school kama wanasheria? Au fafanua madalali wanakuboa kivipi?