Mkuu picha ya hiyo nyumba hakuna?
Habari!
Nyumba inapangishwa, Sinza Makaburini Dar es Salaam
1. Vyumba vitatu, sebule, dinning, jiko, store
2. Haina fence, haina tiles
3. Mtaa mzuri, wa pili kutoka main Shekilango road
4. Kodi 350,000, inalipwa kwa miezi 12.
Mwenye kuhitaji ana PM
Sina picha ila nyumba ni nzuri, muda wowote unaweza kwenda kuiona
huwezi kupokea pesa ya miezi miwilli miwili mkuu?
picha tafadhali, tusije tukapangisha gofu
haina tiles? haina fence? kina lord eyez lazima wasepe na power window zote, kwa maelezo yako tu uliyotoa, hiyo nyumba ni kanyaboya
Acheni uhuni wa kutoza watu kodi miezi 12, huu ni wizi usiovumilika kabisa.
Hv kuna mtu anaelipwa mshahara wa miezi 12 hapa Tz?
Ni serikali inayowapa mwanya wa kufanya huu ujinga wa kudai kodi kwa mwaka mzima. Hakuna sheria ya kuwalinda wapangaji. Nchi nyingi za ulaya ni kinyume cha sheria kutoza kodi kwa zaidi ya mwezi mmoja. Mtu analipa kodi akishapata mshahara.
Siipendi hii tabia ila basi tu nitafanyaje.
Tiba
Serikali inapaswa kuliangalia hili suala, unamlipa mtu kodi ya mwaka mzima halafu yy hiyo hela hailipii kodi hata kidogo.
Watanzania ni wapole sana, kila kitu tunakubaliana nacho tu???
Lakini wanaofanya haya mara nyingi ni hawa madalali uchwara waliojazana mitaani.