NRA kupiga kambi mikoa ya Kusini

hassan kisabya

Senior Member
Jun 14, 2014
165
109
Viongozi wa kitaifa wa NRA watafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini Kwa lengo la kukagua Kazi za chama,baadhi ya viongozi watakaokuwa katika ziara hiyo ni Mhe Rashid Mtuta -Mwenyekiti TAIFA(ambaye pia ni MBUNGE BUNGE MAALUM LA KATIBA),mhe HASSAN KISABYA(N/Katibu Mkuu Taifa na KATIBU MKUU BODI YA WADHAMINI),mhe BAKARI MAANJE(mkurugrnzi Makao makuu Mazingira) na mhe Peter Chipunga(mjumbe bodi ya chama),ziara hii itaanza tarehe 24/06 hadi 29/06/2014.
Ikumbukwe NRA Ndio chama cha kwanza kuonyesha Upinzani wa dhati ktk miaka ya 1994-95, kabla ya kifo cha mmoja wa viongozi wake mashuhuri Hayati Prof.Kighoma Ali Malima,NRA ni miongoni mwa vyama vya kwanza kusajiliwa baada tu ya kuruhusiwa Kwa mfumo wa vyama vingi,kilisajiliwa mwaka 1993,NRA inaamini katika siasa za kistaarabu,siasa zenye tija na siasa za masuluhisho na sio siasa za lawama,fujo ama siasa za chuki,SERA YETU NI "TAIFA KWANZA ,VYAMA BAADAE"
Kwa taarifa hii tunawataka wakazi wa mikoa ya kusini kujipanga kupokea sera nzuri Kwa ustawi wao na kudumisha
amani
 

Mna patikana wapi kiofisi?
 
Hawa Wanaenda huko kuhalalisha ziara za Nnape kuwa hata upinzani walifanya mikutano ..........so wait .....
 
Haki sawa"hizo ni changamoto ndani ya siasa za kiafrika,hatutakiwi kuhofia wengine nao kufanya Kazi za nchi,sidhani kama yupo mtanzania mwenye hati milki ya kufanya siasa,kila chama chenye usajili wa kudumu Tanzania,kitafanya siasa Tanzania na sio China wala Kenya,hivyo tupeane fursa ili watanzania waamue! karibu NRA
 
Last edited by a moderator:

Naona hapa:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…