Hii password mpaka FBI/CIA ya Marekani iliwashinda kuitoa, sasa jiulize wewe mmatumbi utaiweza?
Mpaka sasa cha kufanya ni hiki...
Kama ni yako...
Jaribu kupata password mpya kwa kujibu maswali uliyoweka wakati unafungua account pia uwe unakumbuka email yako... Ikishindwa kama ni yako nenda ofisi za apple wakusaidie.
Kama sio yako...
Mrudishie mwenye nayo au uza kama skrepa kwa mafundi simu!! Tena ufanye haraka maana kama mmiliki ni mjanja anaweza aka search au akaenda polisi watakuja mpaka mlangoni kwako na utakamatwa kama kuku!!
Kwa kifupi mpaka sasa ivi utakua unatafutwa. Ila mkuu kuliko uuze buku 50 skrepa ni bora umrudishie mwenyewe.
BTW NAWAPONGEZA APPLE KWA KUWA ULINZI MKALI KWENYE SIMU ZAO.