Mkuu Ngongo,Mwenyekiti wangu wa kamati ya maendeleo KKKT Mtaa wa Njiro.Tutakukumbuka kwa juhudi zako za dhati za kuhamashisha michango kwaajili ya mabenchi ya kukalia.Unaondoka wakati bado tulikuwa tunakuhitaji sana.
Mungu akubariki kwa kazi nzuri na njema.
Kamanda umemjua lini Ole Njoolay?Ana userious usio na tija.
Hatamaye rais KIKWETE amemteua mh. Daniel Ole Njoolay aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya ARUSHA, MWANZA NA RUKWA KUWA BALOZI WA TZ Nigeria
Kamanda umemjua lini Ole Njoolay?
Naipendaga sana hii nukuu na hasa hapa kwetu imekuwa halisi kupitiliza!hana background ya international relations, watu wenye uwezo na taaluma wapo lakini uchama unatawala zaidi. Siungi mkono makanjanja kutuwakilisha nje ya nchi !!
Mh. JK karudi tu juzi kutoka Austria na kama sikosea theme ya mkutano ilihusu 'new ideas', huwezi jua hii ni katika utekelezaji wa aliyojifunza huko!Watu walio choka mwili na akili ndio wanaenda kuwakilisha nchi! Njoolay anakua balozi kwa lipi jipya alilo nalo??????
Kamanda umemjua lini Ole Njoolay?
Huyu mzee anapenda sana masuala ya uwekezaji. Amefanya makongamano ya uwekezaji katika mikoa ya mwanza na rukwa wakati akiwa mkuu wa mikoa hiyo. Sasa ni muda muafaka wa kutuletea wawekezaji kutoka nigeria waje wafufue uchumi wetu!
Katika hali ya kushangaza aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya ARUSHA, MWANZA NA RUKWA amekaa nyumbani kwa takribani miaka miwili sasa. chakushangaza ni kwamba mkuu huyu ni chapakazi asiye kifani tena asiyependa makuu na vyombo vya habari. Tangu asimamishwe na kuahidiwa kuwa atapewa kazi maalumu hajawa kutokeza hata kidogo kuongelea masaibu haya yalompata mtu huya anayependa maendeleo. Hatimaye tarehe 28/08/2013 rais kikwete amemteua kuwa balozi wa TANZANIA nchini NIGERIA, na uteuzi huu unaanza mara moja. Kitu kingine nachojiuliza ni kwamba kwanini rais amempa STELLA MANYANYA Awe mkuu wa mkoa huo ili hali ni mbunge? lakini mwanaccm huyu mpole amenikosha kwani baada ya kustaafishwa hajakimbilia vyombo vya habari ila alienda nyumba kwake.