Njaa yaendelea kuitesa dunia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Zaidi ya watu milioni 113 walikumbwa na njaa mwaka jana kutokana na upungufu wa kutisha wa chakula kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa na Umoja wa Ulaya na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Hali mbaya kabisa ilishuhudiwa Yemen, Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo, Afghanistan, Ethiopia, Syria, Sudan, Sudan Kusini na kaskazini mwa Nigeria.

Idadi ya watu wanaolala na njaa, licha ya kushuka kutoka ile ya milioni 124 mwaka 2017, bado imeendelea kubwa ya juu mwaka jana, kwa mujibu wa mkuu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO, Jose Graziano da Silva.

Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula, WFP, David Beasley, amesema kuwa ili kukomesha njaa, lazima kukabiliana na vyanzo vyake vikuu, ambavyo ni migogoro, ukosefu wa utulivu, na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwezi Septemba mwaka jana, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalitoa fasili pana ya ukosefu wa lishe, ambapo yalisema watu milioni 821 duniani, sawa na mtu mmoja katika kila tisa, hakuwa na chakula cha kutosha mwaka mwaka 2017
 
Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi yanaonekana kwa uwazi sasa

Jr[emoji769]
 
So sad seeing people starve in different places in the world. And not just that. The wars, the floods, the murders.

Arrrrgh.
 
"Migogoro, ukosefu wa utulivu, na mabadiliko ya tabia nchi"

Haya mambo yataitesa sana dunia ya leo na ya mbeleni... itafika wakati itatulazimi vyakula vitengenezwe mabaara...


Cc: mahondaw
 
Alafu atakuja mjinga kutoka lumumba kukanusha hili,,,, hili jambo lipo wazi kabisa hata baadhi ya mikoa hapa tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…