Nini Hatma ya John Mashaka?


kweli makala ni mazuri sana sana na viongozi wetu wangejaribu kuyasoma
 

Hii makala imejaa makosa ya kiufundi sana, kwanza huyu mwandishi ametoa hoja nyingi na kuziunganisha huku akitoa mfano mdogo kuhalalisha hoja yake. Anaposema watu wanalazimishwa kulipa kwa dola au pesa ya kitanzania inayolingana na dola ni upuuzi mtupu kwani hali halisi ya biashara ndio ilivyo. Nchi nyingi duniani zinapandisha bei ya bidhaa zake kulingana na dola ya marekani. Zamani miaka ya 60 fedha ilijumuishwa na dhahabu, ila ukweli wa leo ni kuwa karibu fedha zote za nchi mbalimbali zinalinganishwa na dola.Anaongea jambo la kipuuzi anaposema mtanzania analazimishwa kulipa kwa dola. Chukulia mfano, mtu unataka kununua tiketi ya ndege kwenda nje ya nchi, na tiketi zao bei zinapanda au kushuka kutegemea na dola, watakutajia bei kwa pesa ya kitanzania na kwa dola itakua uamuzi wako ulipe kwa dola au pesa ya Tanzania, ila lazima uangalie je utapoenda kubadili pesa yako ya kitanzania utatumia pesa nyingi kubadili au kulipa kwa pesa ya kitanzania.
Vile vile anaongelea kuwa ili suala la kutumia dola linaharibu uchumi, ila kama ye angekuwa muelewa angejua kuwa suala la kutumia dola linatumika sana mahoteli ya kitalii, viwanja vya ndege, ofisi za mabolozi nk, na si kila sehemu ya biashara.Na hii si Tanzania tuu bali kila nchi ina mfumo huo kutokana na urahisi wa kubadili pesa na dola ya Amerika ndo inatumika zaidi.Je uchumi wa izo nchi unaharibiwa pia? Je uchumi wa Tanzania ulikua mzuri sana miaka ya 70 au 80 tulipokuwa hatutumii dola kabisa?Hoja yake ni kama vile tatizo la uchumi linasababishwa na matumizi ya dola. Ukienda China matumizi ya dola ya kimarekani ni ya kawaida tuu na raia wengi wanunua dola ili wakawekeze Amerika, je uchumi wa China unaharibiwa kwa kuwa matumizi ya dola ni makubwa?
Suluhisho lake wachaguliwa viongozi amabao watasimamisha utumiaji wa dola, tulikuwa na Nyerere aliekataa kabisa suala la kuwa na dola je uchumi ulikuwa mzuri sana? Ni kipindi icho hata sukari iliuzwa kwa mgao. Huyu mwandishi kama msomi lazima ajue "protectionism" mzuio wa kulinda uchumi wa ndani ikiwa pamoja na kukataa matumizi ya pesa za kigeni hausaidii uchumi. Hoja yake nyingine ya kuwa mahoteli yanamilikiwa na wageni na sio wazalendo ivyo matumizi ya dola ni mabaya kwa kuwa wanaweza peleka pesa zao nje ya nchi ni ya kipuuzi. Kwanza, dunia nzima inaitaji wawekezaji, leo hii mtu mwenye dola milioni moja ankaribishwa Amerika kwa mikono miwili. Kila nchi inataka mwekezaji. Kama wananchi hawana uwezo wa kumiliki hayo mahoteli, serikali ifanyaje? je serikali imiliki? Alijaribu Nyerere akashindwa. Huyu mtoa hoja anshindwa kueleza faida wananchi wa kawaida wanazopata ikiwa ajira, ustawi wa miji iyo na serikali inapata kodi.
Navyojua mtu unapoandika makala lazima utoe chanzo ama sivyo inakuwa kosa la kuigiza "Plagiarization" Kwa nilivyosoma amekua akitumia kitabu cha International Business cha Charless Hill kutoa maana "definition" na kuelezea matokeo yake, sidhani kama aliweka kama chanzo cha habari zake, ama sivyo wengi wetu tunaweza kusema ye ndo kaandika. As an academic I would give him a low grade on this article because it has no good flow of ideas. Too much generalization, and examples which do not support what he wants to infer. His conclusion does not relate to his inference at all. Peace but no hate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…