Nini Hatma ya John Mashaka?

Kuwa mbunge wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania.
 
mwacheni aendelee kwa michuzi.huku position anayodhani inamfaa wameshaikava watu makini kuliko yeye
 
Jamaa hata lugha inampiga chenga halafu watu wanamvulia kofiiiia.

Don't let me murder machete his flow.
 
Amesha shauriwa kuwa aandike kwa kiswahili kama anataka Watanzania wachangie hoja zake na pili akatae kabisa mambo ya kuonekana kuwa anatafuta 'cheap popularity' yaani huko kwa Michuzi utacheka eti watu wanamwita Nabii sijui eti awe Rais wetu na maneno mengi ambayo hakika yanamshusha sana badala ya kumnyanyua au kumweka katika level anayotaka umma umtambue! Nilicheka sana nilipoona mmoja anasema kuwa eti ni yeye mwenyewe anajiandikia hizo comments za kujisifu. Siamini na kama ni kweli basi kujibu swali la mleta hoja ni kuwa hatima ya Mashaka ni kukosa heshima kabisa katika jamii ya Watanzia wanaosoma maandishi yake.
 

Huyu John Mashaka, January Makamba, na Ridhiwani ni wale wale. Huyu tofauti yake na wakina January ni kwamba akili anayo lakini hafai, hawa ndio wakiwpewa nchi wanageuka kuwa wezi wa kutupwa na wakina makamba part 2, kuropoka. Hizi ma upupu zake zisiletwe hapa kwa wasomi, yabie huko huko kwa vilaza wake na michuzi, ambao mashaka kiimba tu, anaitwa Rais mtarajiwa. Ukimkosoa, unaitwa hater. Hater kitu gani bwana, siye watu makini tumetulia tu, hata kusema hatusemi. Mashaka vitendo sifuri ingawa mawazo yake yanajaza sufuria.
 
Wacha wivu wewe...kuandika angalau paragraph moja tu ya Kiingereza sahihi huwezi. Kiarabu ulichokariria aya za Kurani madrassah nacho huelewi. Hata Kiswahili ni kile cha misheni tauni.

Mkuu taratibu!
 

bwana mitusi umerejea na mitusi yako. Habari za mkunazini na Kibanda maiti. milikuona kwenye kampeni zenu za CUF KULE wete.
 

Nilidhania angegombea ubunge, kulikoni au ndo wale CCM imewanunua? Aende Chadema, vichwa kama hivi vinakaribishwa Chadema tu. ila bungeni angekuwa chachu ya vilaza na tiko zake ndefu utadhani minyoo, khaa
 
Hii makala ni nzuri sana, watu bwana, badala ya kushambulia hoja wanashambulia mtu. nafikiri kufanya hivi si kumtendea mtu haki
 
Hii makala ni nzuri sana, watu bwana, badala ya kushambulia hoja wanashambulia mtu. nafikiri kufanya hivi si kumtendea mtu haki

Huyu mkaka hawamtendei haki. Anaandikaga vitu vya maana sana. Slaa akiwa rais, hawa ndio vijana wa kutafuta kuungana na Zitto na Chadema
 

Fisadi Orijino, bwana wewe ni mtu wa mabifu sana.Naona mada zako nyingi ni za jazba sana. Hii atiko imetulia sana, tena ni yenye upeo mkubwa na mpangilio mzuri mno, mbona unamshambulia mwenzio hivyo? jamaa ni kichwa, au hiyo ndo shida yako, subiri sasa tumpigie kura awe rais wako, teteteteteteeeee
 
sikujua wivu ni kwa wanawake tu kumbe wanaume pia mnaoneanaga wivu hehehehehe!makubwa madogo yana nafuu watanzania hatupendani
 
sikujua wivu ni kwa wanawake tu kumbe wanaume pia mnaoneanaga wivu hehehehehe!makubwa madogo yana nafuu watanzania hatupendani

Unaambiwa jamii forum kmejaa wanawake kibao, wivu wazindiki kama nini. john mashaka aende bungeni naye aache kutujazia ukurasa wetu. aingie chadema ndio kuna vichwa siyo ccm
 
Kuna watu wanajifanya wajuaji wa kila kitu humu JF,hii article imetulia haswa na ndio ukweli na uhalisia wa madhara anayoyasema Mashaka.Wakati mwingine inategemea taauluma yako imebase wapi ili uweze kuelewa mambo ya uchumi na fedha kama haya.kwa nini tumponde kwa kingereza chake?wachina,warusi,wajerumani wangapi wanazungumza kiingereza?msiwe na mawazo mgando wa kuelewe wameelewa, waliotoa personal attacks naomba wajifikirie mapungufu yao kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…