Nini hatima ya Zanzibar?


Sahihi mkuu
 
Moja ya sababu zilizolewa na Jecha wakati wa kufuta matokeo yote ya uchaguzi ni kuwa, baadhi ya watendaji ndani ya tume walitofautina na ilifikiwa wakti wakagombana.
Je wajumbe watateuliwa upya kabla ya uchaguzi kufanyika tena ama la. Pili kama watachaguliwa upya ni rais huyuhuyu drCheni ndo atawachagua ama la?
kutokana na katiba ya sasa kuna kipengere kinasema tume katika kutoa maamuzi yake hayataojiwa mahala popoteikiwepomahakamani pia, naomba ufafanuzi pia mwenye ufahamu wa jambo hili kama ikitokea kuwa wajumbe watabadiliswa kabla ya uchaguzi kurudiwa.
 
Imewekwa wazi kuwa CCM haijawahi kushinda uchaguzi mkuu Zanzibar tangia 1995. Nimesoma Mzee Moyo aliweka hilo wazi kuwa Yeye ndio alimfuata Seif akubali "kushindwa" kwa sababu CCM hawana mpango wa kuacha kung'ang'ania madaraka. Kwa hiyo tatizo sio kama Seif alishinda, tatizo ni kuwa CCM wameshashindwa mara inne na hii ni ya tano.

Tatizo si mashabiki, Tatizo ni CCM na Tume isiyo huru ya uchaguzi.

CCM inang'ang'ania madaraka na Tume haitendi haki.


NEC wameiwezesha CCM kwa upande wa bara na ZEC walitegemea kuiwezesha CCM Zanzibar. Seif aliweza kukusanya matokeo yaliyobandikwa vituoni mapema na kuweka wazi kitu kilichoweza kuifunga mikono ZEC isiweze kuchakachua na kuiwezesha CCM.

Kurudia uchaguzi sio tu ni ufujaji wa fedha za umma na wafadhili lakini pia ni ubakaji wa demokrasia wenye nia ya kuibakisha CCM madarakani.

Zinahitajika billioni 12 ili kurudia uchaguzi.

Moyo: Nilitumwa kumshawishi Seif akubali - Kitaifa | Mwananchi

What it’ll cost to repeat Z’bar polls - News | The Citizen

Lipumba aishukia ZEC kufuta uchaguzi Zanzibar - Live Blog | Mwananchi

 
Last edited by a moderator:

sawa nimekusikiza na nimemsikiza Bi Fatma (Mwanasheria), waswahili wanasema kila mwamba ngozi uvutia kwake. Mimi sidhani na sihafiki kwamba CUF walishinda chaguzi zote zilizopita. CUF itakuwa kichwa cha mamluki kukaa tu kimya na kuna ushahidi wameshindwa chaguzi zote hizo, Maana kama ni kweli, CUF wajiulize swali la msingi, je wao kama chama cha siasa wako hapo kuongoza nchi au kuwa wapinzani, na sidhani jibu litakuwa hilo nalowaza mimi...

Kwangu mimi na watu wote na jumuia ya kimataifa kwa ujumla tunaelewa kwamba CUF hawana support kubwa Zanzibar ndio mana hawakuwa na kura za kutosha kwenye chaguzi zilizopita. kama hilo litabadilika huko mbeleni sijui LAKINI uchaguzi huu umefichua tactics zao za ku-rig uchaguzi huu, HAKUNA mtu kutoka CUF aliyepingwa allegations hizo and so, the allegation will stand, at least for now.
 

naomba huyu mama usimuhusishe na hzo siasa zenu sa hivi,kweli alitenda kosa ila sasa hivi ni mgonjwa tunaomba mutuache tumuuguze mpendwa wetu,hzo siasa zisifanye mututajie watu wetu ambao kwa sasa wamejitenga na siasa
 

Mkuu pole sana. Usiwaze sana utaumia bure, hawa jamaa ni kuwasamehe bure tu. Hawana hata chembe ya huruma hata kidogo. Wamelewa madaraka, wamelewa raha za madaraka, na wamesahau kuwa nafasi walizonazo ni dhamana ya wananchi.

Inatia uchungu na huruma, umeongea kwa uchungu sana.

Mwenyenzi Mungu asimame kuwatetea Wazanzibar
 
Nimekusoma na nimefahamu si mfuatiliaji makini wa Siasa za Zanzibar au ni kijana mdogo. Kama utamfikia Mama Samia Suluhu muulize hilo la CCM kutangazwa washindi kwa hisani ya Tume ya uchaguzi na shinikizo la vyombo vya dola. Jambo hilo sio siri.

Kama umemsoma Moyo anataka ushahidi zaidi ya huo?

Angalia video hii dakika ya 2.26 inaipa nguvu makala ya Moyo uliyoisoma.

 
Last edited by a moderator:
Nafikiri matamko yanabadilika.tayari japo tamko linasema matokeo YOTE yamefutwa,tumeambiwa Yale ya urais Wa Jmt naya ubunge Wa jmt ni safi
 
Kwa nini uchaguzi urudiwe Zanzibar tu?

Uchaguzi urudiwe kwa sheria ipi au katiba ipi?

Kwa nini NEC imemtangaza mshindi wa nafasi ya Uraisi huku kukiwa na utata wa uhalali wa uchaguzi kwa upande wa Zanzibar?

Zaidi ni kwa nini Rais mteule aliapishwa huku kukiwa na utata wa uhalali wa uchaguzi Zanzibar?

Vipindi vya uelimishaji wananchi juu ya kilichotokea Zanzibar na mgongano wa kikatiba na kisheria.

 
Last edited by a moderator:
Hata kama Seif Atasusia uchaguzi maccm yataitisha uchaguzi na vibaraka wake wa ADC watajidai wanasimamisha mgombea. Majority watasusia uchaguzi lakini haitarudisha nyuma uhuni wa ccm (refer kura za maruhani za akina Aboud)na mwisho wa siku wakina Jecha watamtangaza Shein kuwa Rais. Watamwaga Jeshi lote huko Znz kuwatisha wananchi na Rais fake wao ataapishwa kibabe.
 
Mkwara wa kuvua shati kabla ya kuzipiga ni wa enzi zile. Wajumbe wa ZeC old school kweli. Anyway minus Jecha ni waadilifu.
 
Hatima ya Zanzibar ipo kwa yule ambae ni mwenye nguvu na mmiliki wa dunia na vilivyomo vya dhahiri na siri,vivyoonekana na vilivyofichikana maana risasi haina uwezo sawa na jiwe.
 

nimefuatilia sana siasa za Zanzibar, tangu kabla ya kufanya mapinduzi. sidhani kama CUF wana wanawapiga kura wengi. jinsi hali ilivyo ni kwamba uchaguzi itabidi urudiwe. the last election was rigged and marred with corruption, the entire process to that fact was rigged hence there will be another election.



tofauti ya kura za CCM na CHADEMA uraisi ni zaidi ya laki 503,765 hiyo ina maanisha hata Zanzibar wakirudia matokeo ya bara hayata kuwa affected, ndio mana uchaguzi utarudiwa ZNZ tu.

Uchaguzi huu utarudi kwa sheria za Uchaguzi kulingana na Katiba ya SMZ ya mwaka 1984.
 
Nimekusoma na naona talking points zako.
Wanaoijua Katiba hiyo ya 1984 wanatoa hoja zao , angalia video. Baada ya kuingalia ,rudi na hoja mbadala.

Vipi umejiridhisha hayo niliyoweka red?

Unadhani?
 
Hakuna uchaguzi unaorudiwa, tatizo kule waafidhina wa ccm kumtoa mmoja wao haongeze nchi na maalimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…