Nini asili ya neno 'Zeluzelu'?

kidole007

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2012
Posts
3,094
Reaction score
1,877
Wataalamu wa lugha ya kiswahili husikeni na kichwa hapo juu. Tumezoea kuwaita ndugu zetu wenye albinism zeruzeru, nini asili (etiology) ya neno hili?
 
Dah mbona mtihani wa kiswahili zelu zelu au zeru zeru
 
Hahahaaaa zelu zelu, r inakusumbua ngoja wataalum waje waanze na ww
 
Kuna mtu alilianzisha ndio ikapewa maana hiyo na ndio mwanzo wake.
 
Lugha nyingi za kibantu hutumia neno zeru, nzeru,izeru nk. Ili kumaanisha nyeupe au enye weupe, so nahic walitumia hilo neno kumaanisha MTU mweupe,
 
ukichunguza utagundua kuwa herufi "eru" ni msingi wa neno linalotumiwa na baadhi ya waongeaji wa kibantu kumaanisha "eupe" (white)

kwa wahaya utapata "rweru" makabila mengine utapata "nzeru" "nderu" "ng'eru" nk...so nina imani kabisa kwa kuwa albino ni weupe (at least kwa umaskini wa majina ya rangi kwenye kiswahili) basi neno zeru zeru litakuwa lina chimbuko lake hapo kumaanisha weupe usiomithilika
 

Umenitoa tongo tongo
 

Umenena vizur japo sina uhahika kma makabila yote yenye asili ya kibantu neno nzeru linamanisha nyeupe
 
Huna uhakika mkuu kidole?
Mbona neno Etiology haujakosea na kuandika Etiorogy?

neno lenyewe zeru zeru sijui kma ni kiswahili rasmi sijawahi kuliona kwenye vitabu zaid ya kulisikia
 
Umenena vizur japo sina uhahika kma makabila yote yenye asili ya kibantu neno nzeru linamanisha nyeupe

Usiwe kichwa ngumu ndugu,hakuna alipoandika makabila yote.Amesema baadhi ya waongeaji wa wa lugha za kibantu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…