Ninasumbuliwa na (tinea fungal infection) dawa za hospitali zimeshindwa kunitibu nisaidieni

Mwigamba son

Member
Jan 11, 2012
27
6
wana JF kama kuna mtu anamfahamu mahali ambapo naweza kumpata daktali bingwa wa ngozi (dermatologist) anitaarifu maana fungus zinatishia maisha yangu . Ni mwaka sasa nimekuwa nikienda hospitali kupimwa na kupewa dawa lakini bado fungus zimeendelea kusambaa. zaidi ya hapo nimechomwa sindano kadhaa lakini tatizo bado.
naombeni mawazo yenu nifanyeje?
 
Inategemea upo wapi maana Dermatologist wanapatikana hospitali zote za rufaa. Hata hivyo ni dalili gani zinazopelekea useme una fungus au ni kipimo gani ulichopimwa na kuthibitisha una fungus? na dawa gani ulizotumia?
 
Kwa sasa hivi uko wapi? Kama uko pande za kaskazini nenda KCMC they have the best dermatologists. Kwa Dar sifahamu vizuri ila kuna thread ya juzi juzi (2 weeks ago) mtu aliomba ushauri wa daktari wa ngozi na akapatiwa majibu mazuri kuhusu madaktari wajuzi wanaopatikana Dar. Itafute
 
Una dalili zipi? Na umetumia dawa gani? nahisi hujatumia dawa sahihi, na pia ni tinea ipi, tinea zipo za aina kulingana na eneo lililopo fafanua zaidi. Fungus nyingi ni vidonge na kupaka sio sindano, vinge hasa km ipo ktk mwili na ni sememu nyingi( systemic infection) na dawa ya kupaka(topical ceams) km ipo sehemu moja.
 
kaka nenda pale tegeta kwa masister,mi juzi nimempeleka ndugu yangu alikuwa na tatizo la kama lako ,akapimwa akaonekana ni fungusi akapewa dawa,akachomwa sindamo, vidonge vya kumeza na dawa za kupaka naona anaendelea vizuri,na huduma yao ni nzurh sana.kama upo dar itakuwa rahisi,nenda tegeta,ukiteremka pale ulizia m2 yeyote ilipo hospitali ya masister,watakuelekeza ni kama mita 150.toka hapo stand.
 
mkuu nami ninatatizo hilo ila fungus wapo sehemu za siri. nitaenda tegeta nikija dar. ahsante
 
kuna doctor mmoja yupo pale dispensary ya chuo kikuu ni doctor wa ngozi na anapatikana kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2 asubuh mpaka saa 6 mchana. ni mzuri sana alinisaidia mimi kwenye maswala ya ngozi na sasa niko powa na gharama zake ni nafuu sana.
 
nystatin sijatumia na ukimwi nilishapimwa mara 4 na matokeo ni hasi wakondya bro (asante)
 
niko mza vipimo nimevipata kutoka bugando hospital. baada ya blood culture, skin scrapping, stool test, urinary test na vdrl dawa nilizoandikiwa na matabibu ni ketokonazole, fluconazole,turbenafine,grisiofluvin,whitefield,sonaderm,v2 plus, usp injection,hydrocortison na si lazima panapo hospitali ya rufaa kuna matabibu bingwa wa magonjwa ya ngozi . Kwa dhati nakushukuru
 
nafikili mimi nizaidi yako kwa maana zilianza mikononi na miguuni sehemu ya ngozi ya juu karibu na kucha na sasa zinaendelea kushambulia kucha za mikononi na miguuni pamoja na viganja. Pole ila na imani ipo siku vitakwisha na tutasahau maswahibu haya. siku njema
 
dah,pole sana kwa tatizo la fungus.jaman na mimi naomba mnisaidie wana-jf coz nna mba kichwan mpaka nakosa raha naomba mnisaidie
 
vipimo kutoka bugando hospital .tinea manuum,tinea unguiuum,& tinea pedis . dawa nilizopewa ni ketokonazole,fluconazole,terbenafine,grisiofluvin, v2 plus,whitefield,sonaderm,hydrocortisone,sulphur,....usp injection yellowish in colour 7 enjections for a week dose, ipo sehemu za juu za vidole vyote miguuni na mikononi na sasa zinatafuna kucha na kuenea kwenye viganja na sehemu za unyayo hali zikitoa majimaji na kuwasha vipo kwa mfano wa vijiduara shukrani Muhubiri
 
Mwanza kulikuwa na daktari bingwa wa ngozi mmoja tu pale sekou toure sema alihama mkoa na hata hapo bugando walikuwa wanamtegemea yeye. Pole sana, mungu akujaalie upone haraka
 
Naona tumia kata Alovera na tumia majimaji yake kupakaa kila sehem iliyoadhirika asubuhi na jioni kwa muda siku saba kama itakuwa bado uliza tena ili tubadlishe dawa ya mitishamba maana ndo nzuri kuliko za kizungu kwani hazina uhakika hasa katika fungus na virus
Kama hakuna pakaa asali iliyochanganywa na kitunguu swaumu sehemu iliyoadhirika kwa muda wa siku saba na ni asubuhi na jioni (Ratio asali unit moja na mchanganyiko unit moja) kama kijiko au kipimo chochote
 
vipimo kutoka bugando hospital .tinea manuum,tinea unguiuum,& tinea pedis . dawa nilizopewa ni ketokonazole,fluconazole,terbenafine,grisiofluvin, v2 plus,whitefield,sonaderm,hydrocortisone,sulphur,....usp injection yellowish in colour 7 enjections for a week dose, ipo sehemu za juu za vidole vyote miguuni na mikononi na sasa zinatafuna kucha na kuenea kwenye viganja na sehemu za unyayo hali zikitoa majimaji na kuwasha vipo kwa mfano wa vijiduara shukrani Muhubiri

Duuh! pole sana kwa masahibu yaliyokupata.inaonekana umeshakutana na ma-specialist wa ngozi lkn bado hujapata nafuu.kama hutajali hebu jaribu kwenda hapo Bugando kisha uwatafute watu wa pharmacy kisha waombe wakutengenezee salicylic acid 15% ya kutosha kisha uwe unapaka baada ya kuichanganya na dawa nyingine za kupaka kama miconazole au isoconazole au tolnaftate ikibidi hata mara tatu kwa siku huku ukimeza strong antifungal tabs pamoja na antibiotics(kwa ajili ya kukausha vidonda/vipele).Pia uwe unaoga kwa kutumia dettol au potassium permanganate.Jaribu hii tiba naamini utaona mabadiliko.
 
kuna Dr, alikuwa Muhimbili miaka ya tisini inasemekana ana clinik yake pale Taki bovu Dsm. sikumbuki vizuri jina lake (may be Dr. Masange not sure) ukiweza kumpata huyo, nina hakika tatizo lako litakwisha. atakuandikia formular kutokana na tatizo lako utaenda mooners watakutengenezea dawa. niliwahi peleka shemeji yangu alikuwa na mba kichwani na hakuota nywele for years, alipona na sasa ana nywele kichwani za kutosha.

Kuna mwingine nilimwelekeza akamuone alikuwa na Fungus sugu miguuni, naye pia alipona.

ukipata nafasi nenda Dar, mtafute huyu Dr. (99% tatizo lako litakwisha)

Ugua pole.
 
Back
Top Bottom