Sweety Juma
Member
- Nov 8, 2013
- 13
- 10
Asante dada nimekuelewa nasema Inshaallah kwa uwezo wa Mungu. Ck njema.... Sweet Juma pole sana kwa upweke ulionao ila nikuambie kitu dada yangu, usithubutu kumtafuta huyo mwanaume kwa presha sana, wewe tulia muombe Mwenyezi Mungu na ninaamini atashusha rehma zake na utampata ambaye unamhitaji..ukifanya kwa haraka sana (desperately), unaweza kupata pasua kichwa akakuumiza tu akili yako..utafanikiwa na ninakutakia kila la kheri inshaallah!
Salam wana JF. Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 48 ambaye naishi na VVU natafuta mwanaume wa kuishi nae au kufunga ndoa, kama yupo tayari. Awe na umri kuanzia miaka 50-55, kwa ufupi nilikuwa na mume ambae nilimuamini na kumpenda sana yeye ni mfanyabiashara nje na ndani ya nchi baada ya miaka 4 alianza mabadiliko ya kutowasiliana tena na mimi. Mwaka uliofuta nilipata mchumba na tulihitaji kufunga ndoa nikaona niende ANGAZA kuangalia afya yangu lakini haikuwa siku nzuri kwangu kwani nilijikuta nimeshapata maambukizo sikuwa na jinsi. Nilimuomba Mungu katika sala zangu anisaidie na kunitia nguvu katika maisha yangu ya upweke. Kwa vile nimezoea kuwa na mwenzangu kuishi peke yangu ni vigumu kwangu, nami naomba kujitokeza mimi nipo katika ukweli (serious) na tutalindana.
Sasa miaka 48,tena mwanamke bado tu unahitaji kuolewa,mbona kama miaka emeenda sana?