*NIMERUKA MTEGO WA PILI NA RAIS MAGUFULI*
*Na Sangu Joseph*
Leo Aprili 22 , 2020 nimemsikiliza kwa makini sana Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na nimeendelea kukujua kwamba ni kiongozi anaeujua uhalisia wa wananchi anaowaongoza.
Majuma kadhaa yaliyopita, nilipita sehemu mbalimbali na kuwauliza wafanyabiashara wadogo wakiwamo mama lishe iwapo wanaweza kumudu maisha bila kufanya kazi kwa kutumia akiba zao tu.
Wachache walinieleza uwezo wao ni wa siku mbili tu huku wengi wao wakisema wanategemea wafanye kazi kila siku ndipo wapate chakula.
Licha ya kelele nyingi za muda mrefu zinazoshinikiza kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wafungiwe majumbani kama hatua ya kuepusha maambukizi ya virusi vya corona, Magufuli amekuja na maamuzi ambayo kwangu nimeyaita kama kuruka mtego wa pili ambao wapinzani wake wangetamani auingie na iwe ngumi yao ya kumpigia hapo baadaye (Soma mtego wa 1 aliouvuka Magufuli
Hata mimi ningefanya kama Rais Magufuli - JamiiForums )
Ni kweli tunajua kwa sasa DSM ndiyo inaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa corona kuliko mikoa mingine kwasababu ya kuwa na mji wa kibiashara wenye idadi kubwa ya wakazi na watu wanaoingia na kutoka.
Nasema Rais Magufuli amevuka mtego huu wa kuifungia Dar kwasababu asilimia kubwa ya Watanzania hawana uwezo kumudu maisha ya bila kufanya kazi zaidi ya siku 5. kuanzia siku 5 na wengine hujua watakula nini baada ya kwenda kutafuta asubuhi.
Endapo Rais angeruhusu _'lockdown'_, maana yake shughuli za kiuchumi na uzalishaji zisingefanyika ndani ya Dar es salaam na hata nje ya DSM kungekua kugumu.
Fikiria wewe ndiyo Rais halafu unawafungia watu milioni sita asilimia ambapo asilimia 80 hawana uwezo wa kuishi zaidi ya siku 5, ungeongozaje?
Hivyo uamuzi wa kulifungia jiji hilo la kibiashara ungepelekea vifo vitokanavyo na njaa, ongezeko la uhalifu, na hata maandamano mithili ya yale yanayoshudiwa huko Marekani.
Hivyo badala ya kuwaponya watu na Corona, tungewaua watu kwa njaa, na matukio ya uhalifu. Kwa uamuzi huu wa Rais Magufuli, kwangu ameruka mtego mwingine nampongeza sana.
*Insta : FB ; Twit : Sangu Joseph*
*#KijanaMzalendo* *#IloveTZ*
Sent using
Jamii Forums mobile app