Nimelia sana usiku wa leo, nipo katika kipindi kigumu sana cha maisha

Aisee umezaliwa mwaka gani ?
 
Nawaza sana,mwezi mwaka huu namaliza masomo yangu, je kipi kitatokea, wadogo zangu watano Wana- nitazama kaka yao wakiwa na matumaini makubwa sana ndani yao juu Yangu

Stress zinataka kuni maliza, nipo scared sana wakuu
Acha upumbavu wewe kijana mdogo. Kwanza kinachokupa stress ni nini wakati hata hayo maisha hujaanza? Kama uko chuo soma kwa bidii furahia uanafunzi wako. Ukiendelea na huu upumbavu wa kujipa stress za kishamba utaishia pabaya.
 
Huyo hata kuajiriwa hafai ataenda kufundisha stress watoto wetu tu mashuleni.

24 unapata stress za ugumu wa maisha ni upumbavu.

Hana mtoto wala mke anajiliza ugumu wa maisha !!!.

Maisha hayajawahi kuwa na huruma na watu dhaifu vichwani.
 
Brow, walau wewe una CV, Me mwenzako situation ya familia ipo kama yako na sina CV yoyote street toka 2017 hadi now nimeweza kujitegemea 100% na kidogo viteniteni naweza kutuma nyumbani wazazi wakilia and just imagine baba na mama walitengana hivyo na-manage pande mbili hivyohivyo Mungu anasaidia na makosa sitokuja kufanya ni kuleta mtoto duniani ikiwa Mungu hajanipa hela ya kufanya mwanangu asijekuomba asingezaliwa kama mimi.
 
Just Chill Son,,b'se GOD ABOVE ALL"Pambana usikate Tamaa,,Kama Wazazi wako Wamepambana na Kukupambania upo na wao bado wapo licha ya changamoto za kimaisha,,Nawe Sasa ni wakati wako wa kupambana na kuwapambania katika changamoto za kimaisha,,Hakuna asie kuwa na changamoto katika haya Maisha,,,Kama umekata tamaa nenda kawatembelee wagonjwa hospitali naamini Utamshukuru sana Mungu na utakuja nishukuru pia.
 
Ningekuwa mimi ndiyo wewe, nisingelia usiku kucha kwa sababu kama hizi ulizozitoa hapa!

Badala yake ningejipiga kifua mara saba, na kujiambia kamwe sitakata tamaa! 😩 Na badala yake nitapambana mpaka mwisho 💪 ili kujikomboa mimi wenyewe, na pia familia yangu; kutoka kwenye hili lindi la umasikini wa kipato, kielimu, na pia kifikra.

Halafu kijana wa kiume unaanzaje kulia lia hovyo! Halafu ni nani aliye kudanganya ya kwamba huko Afrika ya Kusini kuna maisha ya maana?
 
Usiwaze dogo tulia bado mapema jichanganye na mtaa taratibu

jifunze ujuzi mbalimbali muda wako utafika na utaona mafanikio ndugu au wadogo zako sio jukumu lako ni la wazazi wako so tuliza akili

Anzisha njia Kisha utawainua mmoja mmoja

Stop having victim mentality
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…