Nimekuwa na tatizo la Mmba mgongoni kwa muda mrefu

The Infamous

JF-Expert Member
May 11, 2009
731
121
Nimekuwa na tatizo la Mmba mgongoni kwa muda mrefu, zilianza kama mabaka niliyapata nikiwa nafanya mazoezi, benchi nililokuwa nalalia kwenye mazoezi lilinikwangua likaacha michubuko baadae ikageuka kuwa mmba. nimetumia vidonge kwa mwezi mzima, zikaisha, lakini zikarudi tena, nikatumia tena vidonge kwa week mbili na dawa ya kupaka lakini bado zimegoma kuisha.

Napenda kufahamu kama naweza pata dawa mbadala.

AMANI YA BWANA IWE NANYI.
 
zilianza kama mabaka ambayo uliyapata ukiwa mazoezini?

benchi lilikukwangua na kukuachia michubuko baadae ikageuka kuwa mba?

nafikiri inaweza kuwa ni maambukizi uliyoyapata kutoka ktk mazingira yanayokuzunguka,

hasa kwakua umejua ni kutoka ktk sehemu ya mazoezi....ila sio kweli kama mikwaruzo ya benchi imegeuka na kuwa mba,

Inawezekana benchi ulilotumia alianza mtu mwenye hao mba....na wakati wa mazoezi either alikua wazi on top au t-shirt yake ililowana jasho hivyo akaacha hao wadudu kwenye benchi, na wewe ulivyoenda kutumia hilo benchi ukabeba hao mba,

Ingependeza ukaenda hospitali ujue hao mba wapoje ili utumie dawa sahihi....acha kujaribu jaribu madawa bila ushauri wa madaktari.

......IWE NAWE PIA.
 
Back
Top Bottom