Utaelewa tu mkuu - endelea kusoma post za wachangiaji ...Kuna aliyemwelewa?
Nimetoroka, najua wapo wanaonifuatilia lakini tayari nimeishajichanganya kwa wenye uhuru wa kifikra. Sirudi tena kwa wenye mawazo ya kusaidiwa.Njoo na ID yako ya zamani
Ipo siku ... hadi lin mkuu? wanaendelea kuwavisha makofia vijana na wanawake ...Mkuu ipo siku utamaduni huu wa kofia utaisha tu nina imani hiyo na watu wataanza kuona ujinga uliofanywa na wazee wa ukoo katika maamuzi ya mila hizi potofu
Wachache wanaofanikiwa kuitoboa lakini wanaendelea kuwa na vitu kama vilemba; hawatoki humo kwa sababu wana namba za kuwasaidia kuhudumiwa vizuri - ila mawazo yao hayafanyiwi kazi.Kwa nini haukutoboa kofia ili umalize tatizo kwako na kwa wengine ambao hawakustaili kuivaa au kofia ilikuwa ya chuma mkuu.
Mwenye kakofia huyo kaishajitokezaIpo siku ... hadi lin mkuu? wanaendelea kuwavisha makofia vijana na wanawake ...
Kaka nini tena!
Angalia usije ukawa umemkimbia mvesha kakofia....ukaangukia kwa mvua pikyu yako.... duniani tambara bovu ohoo...Kwetu hali ni mbaya sana ...
Kijana ukifikia miaka 15, unavishwa kakofia .. kofia hiyo inakusababishia matatizo makubwa sana. Huwezi kuuliza swali lolote .. na hata ukiuliza ukajibiwa huwezi kujua umejibiwa nini.
Ukishavishwa kofia unakuwa kama mtumwa wa fikra. Anachosema mmiliki wa kofia ndo hicho hicho. Akiamrisha kwenda kuwaua binadamu wenzio - wala huwezi kuhoji - ni kutekeleza amri tu.
Unajua nilifanikiwaje kutoroka huko kwetu ...
Alipatikana mtu mmoja ambaye alikuwa amevaa kofia ile kumbe ilikuwa ni kofia feki. Yeye alikuwa na uwezo wa kuhoji, na wenzake hawakumtambua kuwa kofia yake ilikuwa haifanyi kazi kama za wengine. Huyu ndo mkombozi wa wale ambao hawajavaa hizo kofia.
Kwetu .. sijajua itakuwaje baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
Ebu nikanywe chai kwanza ila nikirudi nitawajuza zaidi kuhusu huko nilikotoka.
Nikaribisheni jamani ... naona hapa kuna uhuru wa kifikra.