Familia nyingi za kiafrika wazazi uwa wanaona ni jambo la aibu kukaa na vijana wao wanaobalehe na kuwapa somo. Badala yake either watakuwa madkteta au watatafuta mtu mwingine kwa niaba yao. Angalau mamako alikuwa na guts za kukupa twisheni. Mimi sikuwahi kupata nafasi hiyo ila dunia imenifunza mengi...
Hivyo unahisi pana kosa hapo? Unafikiri hata hao wazungu kwanini wameweka umri fulani wa kuruhusu mahusiano ya kimwili? Unasema tuko kwenye Transition kuelekea wapi ambapo bado hatujafika? Hii hadithi si kitu chengine bali ni majuto ya huyo alieitowa kwa kuona jinsi jamii ilivyoondoka kule kuzuri ilikokuwa.
Bahati mbaya hatuwa hiyo hatukuipitia na badala yake tumeruka mojakwa moja kwa binti kufanya anavyotaka bila ya ushauri wa wazee. Halafu hawa wazee wetu wamejikuta wakinyanganywa nafasi za kuwafunza mabinti wao na badala yake mafunzo ya mabinti yamo katika mtandao. hao wenzetu wamefika hapa pa kutegemea mtandao baada ya kupitia hiyo hatuwa unayoitamani wewe yaani ya wazazi na wazee kukaa pamoja wakajadili mambo ya ukuwaji wa mwanamke.
Aisee,kwahiyo ndiyo kusema mpaka hivi sasa bado hujabahatika hata kufanya mapenzi kama jamaa alivyo shindwa kusoma alama za nyakati?Ni story nzuri,ila umeikatisha!Hadi sasa hujasema status yako ikoje ili niweze jua the way forward