Safari hii nikiwa kwa babu na bibi, Bariadi- Shinyanga. Siku hiyo tulikuwa tumeandaa msosi kwa ajili ya sherehe fulani. Hii ilikuwa asubuhi, muda wa chai, tupo kwenye foleni.
Nyuma yangu alikuwepo mshikaji mmoja akifuatiwa na mzee fulani anayesifika kwa ulafi. Yule mshikaji alipopewa chai, tena chai ya maziwa, akaanza kulalamika kiutani, "chai yenyewe ya bariiidi kama ya mgonjwa!".
Yule mzee aliyekuwa akimfuatia kwa karibu alipopewa chai yake huku akiamini kweli ile chai ni ya baridi, aliimimina yote mdomoni fasta ili apate nyingine.
Masikini kumbe ile chai ilikuwa moto sana, yule mzee alitema chai yote huku akilia kama mtoto mdogo. Lakini kwa taratibu za Kisukuma, mzazi wa yule kijana alipigwa faini ya jogoo kwa kutokumfundisha mwanae adabu.