Nigeria wanatengeneza magari

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,351
Naona kuna kampuni nyingine inaitwa Immoson, ukiondoa ile ya Kantanka ambayo ni ya Ghana. Hii ni moja kati ya kampuni chache sana za Kiafrika zinazotengeneza magari (sio kuasemble vipuri).

Afrika tuna tatizo la bei kubwa za magari kutokana na usafirishaji (na hulka ya ubeberu ya kutengeneza faida kubwa), wakati tunayo hazina kubwa ya chuma na chuma cha pua.

Wanaojiita viongozi wetu wameshindwa kushawishi kampuni za magari kuja kufungua matawi ya viwanda huku, ili tupate hayo magari kwa bei nafuu.

Ushirika wetu wa kibiashara bado uko na nchi nyonyaji, tumepuuza teknolojia kutoka kwa nchi za kiafrika zilizoendelea na tunakumbatia nchi za mgharibi ambazo malengo yake ya kudumu ni kutengeneza faida tu kutoka Afrika.

Hapa chini ni muhtasari (kwa Kiingereza) kuhusu uzalishaji wa magari nchini Nigeria.

​
 
Last edited by a moderator:
..very nice comment, yaani umesema kitu muhimu Sana ambacho viongozi wetu wameshindwa tekeleza.
 
Viongozi wanakosa ile talent ya kumobilize resources kwa manufaa ya nchi
 
Ni kampuni ya Nigeria au FDI ...sijasoma uzi wote ila najua kuna makapmuni ya magari yanayotengeneza magari Nigeria lakini si ya Wanaigeria...
kama South Africa vile...
 
What a nice move to be emulated by other African countries.Bravo nigeria!
 
mbona nyumbu tunatengeneza yale malori ya kijeshi
 
Ni kampuni ya Nigeria au FDI ...sijasoma uzi wote ila najua kuna makapmuni ya magari yanayotengeneza magari Nigeria lakini si ya Wanaigeria...
kama South Africa vile...

Si uusome sasa kabla ya kutoa comment!! Au swala ni ilimradi ku comment tu.
 
Ata sisi tuna nyumbu sema kwasaiz ipo juu ya mawae soon lama jeshi itaiachia kwa wananchi wenye hela na ujuzi nia na malengo tutafika mbali. Me najitolea kununua hisa zaid ya mia wakiuza.
 
mbona nyumbu tunatengeneza yale malori ya kijeshi

Ndio mkuu, mwanzoni mwa miaka ya 2000 nilipata hizi tarifa za kampuni chipukizi ya Nyumbu, kituo chao kilikuwa kambi ya Nyumbu, Kibaha.

Miaka kadhaa ya kurembelea kambi za jeshi na kuona magari yao mtaani naona tu brand za Ashok Leyland na TATA, sijawahi kuona Nyumbu zaidi ya maoneshoni.
 
Ni kampuni ya Nigeria au FDI ...sijasoma uzi wote ila najua kuna makapmuni ya magari yanayotengeneza magari Nigeria lakini si ya Wanaigeria...
kama South Africa vile...

Ila si kuna transfer of technology?? In the long run hao first workers disseminate information to others

Also FDI pay tax
 
hiyo kampuni ni INNOSON yamnaijeria mweusi kaajiri wakorea kusin wanatengeneza karibu aina zote za magari lakini injini wanaagiza nje waafrika magari used ya mil 5 bei inatushinda sio rahisi kununua mapya hayawezi pungua mil 10 hata yakitoka africa
 
watanzania ni maskini sana labda magari yangekua yanauzwa mil3 hapo wengi tungenunua lakini gari used zuri halipungui mil 10 hata yakitengenezwa mapya hapa bado bei haiwezi shuka kuepuka kupata hasara
 
Mbona naona hii bado ni assembly. Huwezi ku manufacture mpaka uwe na injini yako. Utaona bado wanatumia injini za kuagiza.
 
Mbona naona hii bado ni assembly. Huwezi ku manufacture mpaka uwe na injini yako. Utaona bado wanatumia injini za kuagiza.

Nasikia utengezaji wa ndege hakuna kiwanda kinachounda kila kitu, ni kama kwenye kompyuta ambapo watengenezaji wa prosesa ni Intel na AMD kwa sana, wengine wote wanaagiza kwao.
 
Ni kampuni ya Nigeria au FDI ...sijasoma uzi wote ila najua kuna makapmuni ya magari yanayotengeneza magari Nigeria lakini si ya Wanaigeria...
kama South Africa vile...
Kuna mradi wa magari "NYUMBU" uliokuwa chini ya JWTZ miaka ya nyuma. Nina hakika kama ungeendelezwa leo hii ungekuwa unatengeneza magari bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…