Nimesikitishwa sana na taarifa toka Niger, zinazosema kuwa Rais wa nchi hiyo Tandja Mamadou ametangaza kuwa iwapo mahakama itaendelea na msimamo wake wa kumkatalia kubaki madarakani kwa miaka mitatu zaidi ya muda unaoruhusiwa na katiba basi atafanya emergency power grab! Rais Tandja Mamadou amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 na hivi sasa kipindi chake cha utawala(kikatiba) kinakaribia ukingoni.
Niger ni miongoni mwa nchi zinazosumbuliwa na umasikini uliokithiri. Nchi pia iko ukingoni mwa jangwa la sahara hivyo hata uzalishaji chakula ni wa kusua sua.
Hivi karibuni kumekuwa na matumaini kuwa uchumi wa Niger unaweza kuboreshwa kwa kuchimba mafuta na madini ya dhahabu ambayo wataalam wamebaini yanapatika katika nchi hiyo yenye watu milion 14.5. Hii ni habari nzuri inayoleta matumaini, sio tu kwa Niger bali kwa kila anayejali maisha bora ya binaadamu. Lakini, nini kinafuata baada ya habari ya kuwepo kwa neema? MGOGORO!!!
MIGOGORO!!!
na baadae labda VITA!!!
Conspiracy theory: Kuna ''investors'' wako katika hatua nzuri ya kuclose deal ya kuchukua mafuta na madini ya Niger mara tu yatakapoanza kuchimbwa. Kwa kushirikiana na serikali za nchi zao investors hawa wanampa kiburi Rais Tandja Mamadou kubaki madarakani ili deal isiharibike akuja mtu mwingine.Wanamuhakikishia kuwa ''international community'' iko upande wake!
My Take:
Viongozi wa Afrika waliouza ndugu zetu kama watumwa hatujawalaani mpaka leo. Wengine tunaendelea kuwaheshimu kama mashujaa- Shame on us!!! Viongozi wote waliouza watumwa walaaniwe. Sababu wanazotoa eti mikataba waliyosaini ilikuwa ya kilaghai, kulaghaiwa sio sababu ya kiongozi kuuza watu wake. Huyu Tandja Mamadou naye hata kama kuna wanaompa kiburi, anapaswa kulaaniwa kwa kuiweka nchi yake kwenye pipa la petroli huku akivuta sigara.Kwa mara nyingine tunaona vyombo vya habari (BBC in particular) ikishiriki kuweka mazingira mazuri ya mgogoro. Kitendo cha Tandja Mamadou ambacho kinapaswa kusemwa kuwa sio cha kufaa BBC wanajaribu kukijustify kuwa Tandja Mamadou ameboresha uchumi n.k. Viongozi wa Afrika AMKENI. Chukueni tahadhari kabla mgogoro huu haujawa BALAA KUU. Likitokea BALAA kwanza tutawalaani wale wote wenye dhamana ya kulilinda bara la Afrika- Viongozi wa Afrika.